Thursday, September 5, 2013

DSC_0352Na Baraka Mpenja wa , Mbeya
Klabu ya Mbeya City imeweka wazi kuwa kila inapojiandaa na mechi ya Ligi kuu Soka Tanzania huwa inakaa na wachezaji wake kuwaeleza nani watacheza na nani watabaki, huku wakiweka wazi sababu za wachezaji fulani kutotumika katika mchezo.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Maka Mwalwisyi amelazimika kutolea ufafanuzi jambo hilo kufuatia mashabiki wa klabu hiyo wakati wa mchezo dhidi ya Ruvu Shooting kushinikiza kocha mkuu Juma Mwambusi kumuingiza mchezaji wa klabu hiyo, Kenny Ally huku wakiwazomea wachezaji na kusema endapo watatoa sare hapataeleweka.
“Kenny hakuwepo katika mipango ya mechi ile, lakini mashabiki walikuwa wanashinikiza aingie, kiukweli sisi hatuna tatizo na mchezaji yeyote, cha msingi benchi la ufundi liachiwe kazi yake na kama ifike wakati kazi ya mtu iheshimike”. Alisema Maka.
Maka alisisitiza kuwa bado safari yao ni ndefu, kinachotakiwa kwa sasa ni umoja na mshikamano baina ya wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki wa klabu hiyo ili kufanikisha ndoto zao.
Pia amewaonya wachezaji wa klabu hiyo kuachana na tabia ya kucheza na majukwaa kwani tabia hiyo itawamaliza kisoka  na hawatakuwa wakali kama wanavyodhani.
“Mashabiki wana nafasi yao, lakini wachezaji wanatakiwa kuacha kusikiliza maneno yao bali wanatakiwa kufuata maelekezo ya waalimu wao”. Alisema Maka.
Maka aliongeza kuwa Mbeya City ina wachezaji 28 waliosajiliwa na wachezaji 18 tu ndio wanaotakiwa kutumika katika mechi moja, hivyo wachezaji 10 lazima wasiwepo katika mechi.
Kocha huyo amesisitiza zaidi kuwa inafika wakati wachezaji wote wapo tayari kucheza, lakini lazima wengine wabaki, ila huwa wanawaeleza kuwa ligi bado ni ndefu, wapo watakaoanza kutumika na itafika wakati watapumzishwa na wengine wataingia kibaruani.
Kwasasa Mbeya City inaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa tatu wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya mabingwa watetezi, klabu ya Yanga ya Dar es salaam, mec hi ambayo itachezwa septemba 14 mwaka huu uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video