Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
MABINGWA wa ligi kuu soka nchini England, Manchester United dakika hizi za mwisho mwisho, wamegeukia kwa nguvu saini ya Ander Herrera wa Athletic Bilbao ambaye hapo jana alikaa benchi katika mechi dhidi ya Real Madrid.
Mara zote, Herrera amekuwa akianza kikosi cha kwanza cha Bilbao, lakini kocha wake Ernesto Valverde amesisitiza kuwa kiungo huyo hajaomba kuondoka klabuni hapo.
Akiongea na waandishi wa habari baada ya mechi ya jana,Valverde alisema: “Sihitaji kuwa na wasiwasi kuhusu hali ya Herrera, hajaomba kuondoka”.
Mshituko: Ander Herrara alikaa benchi dakika zote katika mchezo wa Athletic Bilbao dhidi ya Real Madrid
“Naamni hakuna kitakachotoke kesho (leo jumatatu). Mambo yamekwenda vizuri toka mwanzo. Sidhani kama nahitaji kuongea na mchezaji (kumshawishi abakie)”.
“Ni mchezaji muhimu kwetu. Maamuzi yangu ya leo (jana) hayahusiani na ofa yoyote”. Alisema kocha huyo.’
Kiungo huyo raia wa Hispania alihusishwa na ofa ya pauni milioni 25 kutoka Manchester United jioni ya alhamisi ya wiki iliyopita.
Mhispania mwenye kipaji: Herrara, akipambana na kiungo wa zamani wa Tottenham, Luka Modric (juu, kulia) amekuwa muhimu sana La Liga
Mtego wa kiangazi: David Moyes (juu) amepiga juhudi kubwa kuleta kiungo, lakini bado anavutiwa na Marouane Fellaini (chini)
0 comments:
Post a Comment