Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
Manchester
United leo hii wamepokea kipigo kikali zaidi katika dimba la the Etihad
tangu mwaka 2004 baada ya kula 4-1 kutoka kwa wenyeji Manchester City.
Kwa
matokeo ya leo, vijana wa David Moyes, Man United wameshuka mpaka nafasi
ya nane katika msimamo wa BPL wakijikusanyia pointi 7 kibindoni, wakati
Man City wenyewe wanabakia nafasi ya tatu wakiwa na mzigo wa pointi 10.
Nafasi
ya kwanza kwa sasa inashikiliwa na washika bunduki wa kaskazini mwa
London, klabu ya Arsenal chini ya kocha Mfaransa, Aserne Wenger wakiwa
na pointi 12 sawa na Tottenham Hospurs wenye alama 12 sawa na Gunners
katika nafasi ya pili, lakini wanatofautiana mabao ya kufunga na
kufungwa.
Mshambuliaji
hatari, Raia wa Arjentina, Sergio Aguero ametikisha nyavu mara mbili,
huku nguli kutoka Ivory Coast, Yaya Toure na Mfaransa, Samir Nasri
wakijipigia moja moja na kufanya kocha wa City Manuel Pellegrini aibuke
kidedea katika mechi ya kwanza ya watani wa jadi wa jiji la Manchester
nchini England, ` Manchester derby`.
Kikosi
Manchester City: Hart 7, Zabaleta 7, Kompany 7, Nastasic 7, Kolarov 7,
Jesus Navas 8 (Milner 71 6), Toure 8, Fernandinho 8, Nasri 9, Aguero 8
(Javi Garcia 86), Negredo 8 (Dzeko 75).
Kikosi
cha Manchester United: De Gea 5, Smalling 6, Ferdinand 6, Vidic 5, Evra
6, Carrick 6, Fellaini 5, Valencia 5, Rooney 6, Young 5 (Cleverley 51
6), Welbeck 6.
Mkali wa leo: Sergio Aguero amejipigia mawili katika ushindi wa City
Bao la kwanza: Aguero akifunga bao lake la kwanza katika ushindi mnono wa 4-1
Mwafrika anayeujua mpira: Yaya Toure akipiga bao na kufanya ubao usomeke 2-0 kipindi cha kwanza
Mzee wa kazi: Yaya Toure akishangilia bao lake
Wazee
kimenuka!: Wayne Rooney, Danny Welbeck na Michael Carrick wakiwa hawana
hamu baada ya mvua kuendelea kuwanyeshea leo Etihad
Dogo tulia, hapa kazi tu!: Marouane Fellain akionesha maujanja mbele ya Yaya Toure na nahodha Vincent Kompany
MECHI ZA LEO NA MATOKEO KWA UFUPI
Finished
|
Crystal Palace
|
- |
Swansea
|
(0-1) | ||||||
Finished
|
Arsenal
|
- |
Stoke
|
(2-1) | ||||||
Finished
|
Cardiff
|
- |
Tottenham
|
(0-0) | ||||||
Finished
|
Manchester City
|
- |
Manchester United
|
0 comments:
Post a Comment