Saturday, September 7, 2013



Miss1
MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro imeanzishwa kisheria kama Eneo la matumizi mseto ya ardhi ikiwa na shughuli tatu kuu.  Shughuli hizo ni:
  1. 1. Uhifadhi wa maliasili katika Eneo la Hifadhi;
  2. 2. Kuendeleza wenyeji na shughuli zao za ufugaji;
  3. 2. Kuendeleza utalii.
Katika shughuli za kuendeleza utalii, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro hutoa maeneo ya uwekezaji wa mahoteli, kambi za kudumu na kambi za msimu za kulala wageni.
Kumekuwepo na taarifa potofu kwenye vyombo vya habari kuhusu ugawaji wa vitalu kwenye Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.  Taarifa hizi ni potofu kwa kuwa Mamlaka haihusiki na ugawaji wa vitalu. Jukumu hilo ni la Idara ya Wanyamapori.
Aidha, katika taarifa zilizolipotiwa, Kampuni ya Leopard Tours imetajwa kupewa kitalu, jambo ambalo siyo kweli.  Leopard Tours imepewa “Special Campsite” ambayo amekuwa akiitumia siku zote – Ndutu Extra kutoka mwaka 2005 hadi sasa.  Alikuwa akiitumia kama “Season Campsite” kwa zaidi ya miezi 5 – 8 kwa mwaka.
Kilichofanyika ni kuipatia nafasi zaidi Leopard Tours itumie kambi husika kama “special campsite”.  Uamuzi huu ulizingatia kuwa Kampuni hii ni mdau mkubwa wa shughuli za uhifadhi kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwani pato la Mamlaka huchangiwa kwa asilimia kumi (10%) na Kampuni hiyo ikifuatiwa na Kampuni ya Ranger Safari ambayo huchangia asilimia sita (6%).  Kwa maana nyingine Leopard Tours ndiyo kampuni inayoleta wageni wengi Hifadhi ya Ngorongoro kulinganisha na Kampuni nyingine zinazochangia.  Kampuni nyingine zinachangia asilimia tatu (3%) hadi 0.13% kwa mwaka.
Aidha ieleweke kuwa, kwa mujibu wa taratibu za uwekezaji za Mamlaka, eneo lenye ukubwa wa ekari kumi ambalo alipaswa kupewa mwekezaji Fazal wa Leopard Tours lilipaswa kulipiwa kiasi cha dola elfu sitini (60,000), hata hivyo Fazal alipewa eneo linalokaribiana na nusu ya eneo alilostahili kupewa.
Kutokana na hilo, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro iliamua mwekezaji huyo alipe nusu ya pesa aliyopaswa kulipa ambayo ni dola za Marekani elfu thelathini (30,000).
Hivyo basi Mamlaka inasisitiza kuwa taarifa zilizolipotiwa kwenye vyombo vya habari kukusu mwekezaji huyu zilipotoshwa.
KAULI MBIU YETU
“UTALII UANZE NA MTANZANIA KWANZA”
ImetolewanaKaimuMhifadhi
MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video