Malkia
wa Zouk nchini Hafsa Kazinja akiwa na Omari Mkali (kushoto) na Abdul
Salvador baada ya kukamilisha kurekodi wimbo wa ‘NIMUOKEOE NANI’ katika
Studio za OM Productions jijini Dar es salaam wikiendi hii.
Malkia
wa Zouk nchini Hafsa Kazinja akirekodi wimbo wa ‘NIMUOKEOE NANI’ katika
Studio za OM Productions jijini Dar es salaam wikiendi hii.
……………………………………………………………………………
Baada ya ukimya wa
muda mrefu, Malkia wa Zouk Tanzania, Hafsa Kazinja, anaibuka upya
katika fani akiwa na ingizo lake la kwanza kati ya kumi aliyoandaa kwa
kuimba wimbo maarufu wa NUTA Jazz Band uitwao “NIMUOKOE NANI”
anauouleta hewani katika mahadhi ya Zouk.
Hafsa Kazinja
anasema ameamua kurudi ulingoni kwa kutoa wimbo huo ili kumuenzi Mzee
Muhidin Maalim Gurumo ambaye amestaafu rasmi fani ya muziki baada ya
kufanya kazi hiyo akiwa na bendi mbalimbali tokea mwaka wa 1960.
“Nimeamua
kuimba wimbo huu wa “NIMUOKOE NANI” ili kumuenzi gwiji huyu wa muziki
kwani wakati yeye anastaafu na mimi ndiyo naibuka upya baada ya kukaa
kimya kwa muda”, anasema Hafsa ambaye alitoka kwa wimbo wake wa “PRESHA”
aliomshirikisha Banana Zorro.
Hafsa ameandaa
wimbo huo wa “NIMUOKOE NANI” katika studio za OM Productions ya jijini
Dar es salaam chini ya wanamuziki nguli, Abdul Salvador na Omari Mkali.
“Nafurahi
kwamba wimbo wa NIMUOKOE NANI nimeuimba baada ya kupata Baraka zote toka
kwa mtunzi na mwimbaji wake Mzee Gurumo mwenyewe.
“Haikuwa rahisi
kama inavyoweza kudhaniwa kwani baada ya kwenda kumuona nyumbani kwake
alinifanyisha mtihani wa kuuimba wote kabla ya kuridhika maana alisema
asingefurahi kuona wimbo wake unaimbwa hovyo hovyo na kuharibiwa radha
yake”, anasema Hafsa, ambaye hivi sana anamalizia ngoma zake zingine
tisa alizotunga mwenyewe, kabla ya kuvamia anga kwa mara ingine.
Hafsa anasema
katika ukimya wake amekuwa akifanya utafiti na kujifunza kwa undani
zaidi fani ya muziki, akipata mawaidha maridhawa toka kwa wanamuziki
nguli ndani nan je ya nchi wakiwemo Muhidin Maalim Gurumo, Omar Mkali,
Abdul Salvador na Lokassa ya Mbongo wa Congo aliyekutana na kufanya naye
kazi alipokuwa ziarani Marekani hivi karibuni.
Msanii huyu wa
kizazi kipya anasema ataitambulisha rasmi ngoma ya “NIMUOKOE NANI”
katika tamasha la kumuenzi Mzee Gurumo lililopangwa kufanyika OKtoba 1,
2013 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
“Natumaini
wapenzi wa muziki watafurika kwa wingi kwenye tamasha hilo name naahidi
kuitendea haki ngoma ya “NIMUOKOE NANI” hivyo wasikose kuja kujionea
wenyewe jinsi sie wa kizazi kipya tunavyoweza kufanya kazi na wakubwa
wetu wa kazi, anaongezea Hafsa ambaye pia anaandaa video yake pamoja na
ya ngoma zake zingine mpya.
Mkongwe Abdul
Salvador, ambaye alikuwa mmoja wa waanzilishi wa bendi ya TANCUT ALMASI
YA Iringa iliyotamba na mtindo wake wa “FIMBO LUGODA”, anamtaja Hafsa
kazinja mmoja wa wanamuziki wa kike waliojaaliwa sauti nzuri na kipaji
cha hali ya juu hapa nchini.
“Kwa kuweza
kuimba wimbo wa Mzee Gurumo na kupatia kisawasawa inadhihirisha kwamba
Hafsa ni mwanamuziki aliyekomaa maana si mchezo kuimba nyimbo ya
wakongwe kwa ufasaha kama alivyofanya Hafsa.
“Na hii
inadhihirisha kwamba uwezekano wa kizazi kipya na cha zamani kufanya
kazi pamoja ni mkubwa sana na sioni kwa nini isiwe hivyo”, anasema
Salvador.
Omari Mkali,
aliyetamba na bendi ya CHUCHU SOUNDS, chini ya marehemu Yusuf Chuchu,
naye anamwelezea Hafsa Kazinja kama moja ya majembe ya muziki hapa
nchini kwa upande wa kinamama, na kwamba anaweza kufika mbali endapo
kama moto aliokuja nao upya atauendeleza.
0 comments:
Post a Comment