Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
BAO la Daniel Sturridge katika dakika ya mapema ya 4 limetosha kuwanyanyua wekundu wa Anfeild, Liverpool katika uwanja wao wa nyumbani dhidi ya mabingwa watetezi, Mashetani wekundu, Manchester United na kuanza ligi kuu soka nchini England kwa ushindi wa asilimia 100.
Kikosi cha Liverpool leo: Mignolet 6; Johnson 6 (Wisdom 78, 5), Agger 7, Skrtel 7, Enrique 6; Henderson 7, Lucas 6, Gerrard 7; Aspas 6 (Sterling 60, 6), Sturridge 7, Coutinho 8 (Alberto 84).
Wachezaji wa akiba: Jones, Ibe, Kelly, Flanagan.
Mfungaji wa bao: Sturridge 4
Aliyeoneshwa kadi: Aspas
Kikosi cha Man United: De Gea 6; Jones 5 (Valencia 37, 6), Ferdinand 7, Vidic 6, Evra 6; Carrick 5, Cleverley 7; Young 5 (Nani 62, 6), Welbeck 6, Giggs 6 (Hernandez 75); Van Persie 5.
Wachezaji wa Akiba: Anderson, Smalling, Lindegaard, Buttner.
Walioneshwa kadi za njano: Cleverley, Van Persie, Carrick, YoungManagers:
Mwamuzi: Andre Marriner 7
Mshabiki: 44,411
Mchezaji bora wa mechi: Philippe Coutinho
Siku ya leo ni mbaya sana kwa kocha wa Manchester United, David Moyes ambaye anatetea taji ambalo kocha mstaafu wa klabu hiyo, Sir Alex Ferguson alitwaa msimu uliopita.

David Moyes ameshindwa kupata ushindi wa kwanza Anfield kufuatia kushindwa kushinda katika mechi 12 alizocheza katika dimba hilo akiwa na klabu yake ya zamani ya Everton.
Hali ni mbaya zaidi kwa Moyes, kwani Wayne Rooney atakaa nje ya dimba kwa wiki chache zijazo kutokana na kuumia kichwa katika mazoezi ya jana, na dirisha la usajili linafungwa kesho usiku na Moyes bado anahitaji kusajili kwa mara ya kwanza.






Finished
|
West Bromwich Albion
| 0-2 |
Swansea
|
0 comments:
Post a Comment