WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – AJALI YA MAGARI MANNE KUGONGANA NA
KUSABABISHA VIFO.
|
§ MNAMO
TAREHE 26.09.2013 MAJIRA YA SAA 06:45HRS HUKO KATIKA MTEREMKO WA PIPE
LINE INYALA BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA
MBEYA. GARI T.605 AXX /T.480 CAX AINA YA SCANIA LORI LIKITOKEA NCHINI
ZAMBIA KUELEKEA DAR – ES SALAAM LIKIENDESHWA NA DEREVA WILSON MACHA,
AKIWA NA TINGO WAKE JUMA S/O SALEHE WOTE WAKAZI WA DSM [AMBAO KATIKA
AJALI HIYO WOTE WAMEFARIKI DUNIA] LILIGONGA KWA NYUMA GARI T.548 BLY/
T.974 BVN AINA YA SCANIA LORI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA SAMWEL
ARON, MIAKA 30, MBENA, MKAZI WA SINZA, KISHA GARI HILO LILILIGONGA GARI
T.876 BKV/T.465 BQU AINA YA IVECO LORI AMBALO LILIKUWA LIMEEGESHWA
PEMBENI YA BARABARA LIKIWA LIMEHARIBIKA, LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA
DEREVA SAMWEL KASUSU, MIAKA 37, MJITA, MKAZI WA GONGO LA MBOTO DSM.
§ AIDHA
GARI HILO T.605 AXX /T.480 CAX LIKIWA LIMEPOTEZA MWELEKEO LILIGONGANA
USO KWA USO NA GARI T.255 AKV/T.272 CDZ AINA YA SCANIA LORI LILILOKUWA
LIKITOKEA DSM KUELEKEA MBEYA MJINI AMBALO LILIKUWA LINAENDESHWA NA
DEREVA SIXTUS S/O KAPINGA, MIAKA 35,MNGONI, MKAZI WA DSM AMBAYE
ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO NA MWILI WAKE KUTEKETEA KWA KUUNGUA MOTO.
§ KATIKA
AJALI HIYO MAGARI MAWILI T.605 AXX /T.480 CAX NA T.255 AKV/T.272 CDZ
YOTE YAMEUNGUA VICHWA NA KUTEKETEA NA GARI T.548 BLY/ T.974 BVN
LILIUNGUA KIDOGO SEHEMU YA KICHWA UPANDE WA KULIA.
§ CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI T.605 AXX /T.480 CAX.
§ MOTO ULIZIMWA KWA USHIRIKIANO KATI YA KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI NA WANANCHI.
§ MIILI
YA MAREHEMU WILSON MACHA NA JUMA SALEHE IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA. JITIHADA ZA KUUTOA KATIKA GARI MWILI WA MAREHEMU SIXTUS
S/O KAPINGA PAMOJA NA KUTOA MAGARI ENEO LA TUKIO ZINAENDELEA.
§ KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA
KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed By:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
PICHA NA MDAU W MBEYA YETU
|
0 comments:
Post a Comment