Friday, September 27, 2013


Diwani wa Kata ya Katuma akitoa mafafanuzi kuhusiana na hoja ya kuhamishwa kwa kijiji cha Bugwe kwa kile kilichodaiwa kuwa kinachangia katika uharibifu wa mazingira. Kwa waliokaa ni wajumbe wa baraza la madiwani wakifuatilia hoja ya mwenzao. MUHTASARI SAINMadiwani wa Halmashauri ya wailaya ya Mpanda wakiwa kwenye vikao vyao vya kawaida vya maamuzi vya Mabaraza kujadili maendeleo ya  mstakabali ya watu wake na Taifa kwa ujumla.

Na Kibada Kibada –Mpanda Katavi.
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kwa kauli moja limepinga maamuzi ya   kukihamisha na pengine kukifuta kabisa  Kijiji cha Bugwe kilichopo katika Kata ya Mpandandogo Wilayani Mpanda kwa kile kilichoelezwa kuwa kinachangia katika uharibifu wa mazingira.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye kikao hicho Diwani wa Kata ya Mpandandogo Hamadi Mapengo,Diwani wa Kata ya Katuma  Mhe Msemo,Diwani wa Kata ya Sibwesa Gaudesi Lusambo, na Diwani wa Viti Maalum Kata ya Mwese Teodora Kisesa walipinga kuhamishwa kwa kijiji hicho wakidai kuwa walijiridhisha kuwa wananchi wa kijiji hicho hawahusika katika kuchangia uharibifu wa mazingira .
Hata hivy walishauri  kuwa watu waliovamia maeneo yasiyoruhusiwa yaliyotengwa na yale maeneo ya   vyanzo vya maji   wafugaji waliovamia maeno hayo kinyume na sheria  kutoka mikoa ya  Shinyanga kupitia mto ugala  na kuharibibu mazingira kwenye vyanzo vya maji waondolewe kuliko kuwaondoa wananchi waliokutwa katika kijiji chao na wameishi hapo miaka mingi na walisajiriwa kisheria..
Kijiji cha Bugwe ambacho kimesajiliwa mwaka 2011 kina  kaya 322 zenye wakazi wapatao 2049 kati yao wanaume 1044 na wanawake 1005 kwa mjibu ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ambapo hata hivyo inadaiwa kuwa wapo watu wengi ambao hawajahesabiwa katika zoezi hilo la sense hivyo inakadiliwa kuwa na wakazi wengi zaidi ya idadi iliyolasimi.
Kijiji hicho cha Bugwe kinadaiwa kuwa kinazunguukwa na mito mingi ambayo ndiyo tegemeo la wakazi wa wilaya ya Mpanda kutokana na maji yanayotiririka kutoka kwenye vyanzo vya mito iliyoko kwenye kijiji hico cha Bugwe kama inavyodaiwa na wataalam wa Idara ya adhi kuwa wananchi wa Bugwe wanachangia kuharibu mazingira.
Akizungumza katika kikao hicho Mbunge wa jimbo la Mpanda Vijijini ambaye naye ni sehemsou ya baraza la madiwani Moshi  Selemani Kakoso alikieleza kikao cha Madiwani kuwa anaungana na maamuzi ya Baraza la Madiwani la kukataa kukihamisha au kukifuta kijiji cha Bugwe kwa kile kilichoelezwa kuwa kiko kwenye vyanzo vya maji na kinachangia uharibifu wa mazingira.
Mbunge huyo alieleza kuwa vyanzo vya maji vinavyozungumziwa viko umbali mrefu kutoka kijiji kilipo cha Bugwe,na eneo hilo ni moja ya eneo nzuri sana na ni eneo oevu kutokana na mazingira yake yanaonekana kama yale yaliyoko hifadhi ya ngorongoro na ni eneo lililoko katikakati ya  Tarafa ya Kabungu na Tarafa ya Mwese.
Na eneo hilo limevamiwa na wavamizi wafugaji kutoka mikoa ya jirani wakiwa na mifugo ambayo wanaipitisha  mifugo kupitia mto ugalla wakitokea mikoa ya jirani, na kuvamia maeneo ya vyanzo vya maji ambavyo ni vyanzo vya mito ya lugufu,katuma,mto mnyamasi,mto lwegele,mfwisi,mto lufilisi na mto lwega na baadhi ya mito inamwaga maji katika ziwa Tanganyika.
Kikao kilitoa maamuzi ya  kutokukifuta kijiji cha Bugwe badala yake Serikali ikawaondoe wale wavamizi wa vyanzo vya maji ambao wanaishi kule wakiwa na makundi makubwa ya mifugo ambayo inachangia uharibifu wa mazingira.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Estomih Chang’ah akizungumzia suala la kuhamishwa kwa kijiji cha Bugwe alieleza kuwa suala hilo liliagizwa na ngazi ya mkoa baada ya kupokea maagizo kutoka ngazi ya wilaya na lilikuwa limeisha jadiliwa kwenye ngazi ya Halmashauri.
Mkurugenzi ameliomba baraza limwagize Mkurugezi awasilisiliane na Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Mhandisi Emanuel Kalobelo iundwe timu ya mkoa wa itakayoenda huko kuona na kujiridhisha katika maeneo yanayodaiwa kuwa ni vyanzo vya maji vimevamiwa na wananchi wa Kijiji cha Bugwe.
Kwa kauli moja Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Yasini Kibiriti alirithia kwa kauli moja maamuzi ya Kikao cha madiwani kupinga kuhamisha na kufutwa kwa kijiji cha Bugwe kwa kuwa kufanya hivyo itakuwa kuwaonea wananchi na watakuwa hawajatendewa haki kwa kuwa hawahusiki katika uharibifu wa mazingira  wao ni rafiki wa kutunza mazingira.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video