Kocha wa Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bora, Ernie Brandts akisalimiana na THEOPISTA JEROME, Msaidizi wa meneja wa kiwanda cha TBLMbeya
Mlinda mlango wa Yanga, Deogratius Munish “Dida” akitazama mtambo wa kupikia bia
Mfanyakazi wa TBL Mbeya, ROBERT ANDREW akiwaelekeza wachezaji


Na Ibrahim Kyaruzi, Mbeya
WACHEZAJI wa Yanga inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager leo
wamefanya ziara kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kilichopo
maeneo Iyunga. Katika ziara hiyo mjini Mbeya na kujionea mambo
mbalimbali, ikiwemo mfumo mzima wa utayarishwaji bia hadi kupakiwa
tayari kuingia sokoni.
Walipata
fursa ya kuuliza maswali mbalimbali wakati wanatembezwa kwenye kiwanda
hicho na wafanyakazi wa TBL Mbeya na kwa ujumla ilikuwa ziara yenye
maufaa kwao.
Wafanyakazi
wa TBL Mbeya walifurahi kukutana na wachezaji wa Yanga na wengine
walichukua fursa hiyo kupiga nao picha za ukumbusho.
Kwa
upande wake, Meneja Matukio wa Kampuni hiyo mjini hapa, Godfrey
Mwangungula alisema kwamba kiwanda cha TBL Mbeya kinashikilia tuzo ya
kiwanda bora cha bia Afrika kwa miaka mitatu mfululizo hivyo ni faraja
kwao kutembelewa na mabingwa wa Tanzania.
Yanga
kwa pamoja na wapinzani wao wa jadi, Simba SC na timu ya soka ya taifa
ya Tanzania, Taifa Stars- wote wanadhaminiwa na bia ya Kilimanjaro
Premium Lager inayozalishwa na TBL.
Yanga
iko hapa Mbeya tangu Jumatano kwa ajili ya mechi zake mbili za Ligi Kuu
dhidi ya timu za hapa. Mchezo wa kwanza ilicheza Jumamosi Uwanja wa
Sokoine na kulazimishwa sare ya 1-1 na Mbeya City wakati keshokutwa
itahitimisha mechi zake za hapa kwa kumenyana na Prisons kwenye Uwanja
huo huo.
0 comments:
Post a Comment