Mkuu
wa mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo (Mwenye suti nyeusi) akikata
utepe kuashiria ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Utalii duniani
yanayofanyika Kitaifa mkoani Mwanza.
Eng.
Evarist Ndikilo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza akitia saini kitabu cha wageni
katika banda la Wizara ya Maliasili na utalii wakati akitembelea mabanda
ya maonesho katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza muda mfupi baada
ya kufungua maadhimisho ya siku ya utalii duniani yanayofanyika Kitaifa
mkoani Mwanza. Kulia kabisa ni Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Utalii
Bibi Uzeeli Kiange.
Afisa
Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania –TTB Bw. Geofrey Tengeneza
akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo namna
Bodi hiyo ya Utalii inavyotekeleza majukumu yake.
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo ameipongeza Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) kwa kufungua ofisi jijini Mwanza kwa kuwa hatua hiyo
itaharakisha maendeleo ya sekta ya utalii mkoani Mwanza na Kanda ya ziwa
na amewataka wananchi wa Mwanza kukuza utalii wa ndani kwa kutembelea
vivutio vya utalii vilivyopo Mwanza, Kanda ya ziwa na Tanzania kwa
ujumla na kuondokana na dhana kuwa utalii ni kwa ajili ya wazungu tu.
Eng.
Evarist Ndikilo amayasema hayo wakati akizindua maadhimi misho ya siku
ya Utalii duniani ambayo kitaifa mwaka huu yanafanyika mkoani Mwanza
katika uwanja wa Nyamaga. Amesema mkoa wa Mwanza una vivutio vingi sana
vya utalii ingawa bado havijatangazwa kikamilifu lakini kufunguliwa kwa
ofisi ya Bodi ya Utalii Tanzania, kupata fursa ya kuandaa maadhimisho ya
siku ya Utalii duniani kwa mara ya pili mfululizo pamoja na ujenzi wa
uwanja mpya wa Kimataifa wa ndege wa Mwanza ni masuala ambayo
yatachagiza maendeleo ya sekta ya Utalii mkoani Mwanza na Kanda ya ziwa
kwa ujumla.
Pamoja
na hayo mkuu huyo wa mkoa ameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii
kushirikiana kwa karibu sana na Chama cha Utalii Mkoani Mwanza (MTA) na
akasisitiza umuhimu wa kuwashirikisha waandishi wa habari wa mkoani
Mwanza katika kusaidia kutangaza vivutio vya mkoa huu na kanda nzima ya
Mwanza “ Niiombe Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikiana kwa karibu
na MTA na wadau mbali mbali wa sekta ya utalii mkoani Mwanza bila
kusahau kuwashirikisha wandishi wa habari kwani kalamu zao zitatusaidia
sana katika kutangaza vivutio vyetu vya Mwanza na kanda ya ziwa” alisema
Eng. Ndikilo
Akizungumzia kauli mbiu ya maadhimisho hayo isemayo “Utalii na Maji kulinda hatma yetu”
Mkuu huyo mkoa amesema ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda vyazo vya
maji na kuhakikisha kuna kuwa na matumizi sahihi na endelevu ya maji
kwani maji ni muhimu sana kwa maendeleo ya sekta ya utalii. Amedokeza
kuwa kwa mujibu wa takwimu za shirika la Utalii duniani UNWTO matumizi
ya maji duniani yanatarajiwa kuongezeka maradufu kutokana na kuendelea
kuongeza kwa watalii duniani na miundo mbinu mbalimbali ya sekta ya
utalii duniani.
Mapema
mkuu huyo wa mkoa ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi aitembelea mabanda
ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Maji, taasisi za Serikali,
Mashirika ya Umma na binafsi na wadau wa sekta ya utalii wanaoshiriki
maonesho hayo kutoka Dar es salaam, Mwanza, Kagera, na nchi jirani ya
Uganda.
Maadhimisho
hayo yatafikia kilele chake Septemba 27, 2013 ambayo ndiyo siku ya
Utalii duniani, lakini yatahitimishwa tarehe Sptemba 29, 2013.
0 comments:
Post a Comment