Na Mwandishi wetu
Nani
atatwaa taji laMiss Universe Tanzania, jibu la swali hilo litajulikana
leo (Ijumaa) wakati warembo 15 kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania
watakapochuana kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini kuanzia saa
moja kamilli usiku.
Warembo
hao mbali ya kuwania taji la Miss Universe Tanzania ambalo kwa sasa
linashikiliwa na Winfrida Dominique, pia watawania taji la Miss Earth
Tanzania na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya
kimataifa.
Warembo
hao kwa nyakati tofauti waliokuwa wakitambiana huku kila mmoja akisema
atatwaa taji hilo na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia
yaliyopangwa kufanyika Novemba 9 jijini Moscow, Russia.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Compass Communications inayoandaa mashindano hayo, Maria
Sarungi alisema kuwa kila kitu kimekamilika na warembo wamepania kufanya
makubwa jukwaani . Maria alisema kuwa warembo wote wana ari ya juu na
kila mmoja akiwa na shauku ya kutwaa taji hilo.
“Kwa
upande wetu, kila kitu kipo tayari, warembo wamejiandaa vilivyo na
tumeandaa shoo bora na fupi, hivyo mashabiki wa masuala ya urembo
wanatakiwa kufika mapema ili kuona nani anatwaa taji na kupata tiketi ya
kuiwakilisha nchi kimataifa,” alisema Maria.
0 comments:
Post a Comment