Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
HOMA
ya pambano kali hapo kesho ligi kuu soka nchini England baina ya
Tottenham Hospurs dhidi ya Chelsea, zote za London katika dimba la White
Hart Lane inazidi kupamba moto, huku makocha wa timu hizo wakitupiana
maneno ya kejeli kati yao na kikubwa ni kukosoana aina ya mpira
unaochezwa na timu zao.
Kocha
wa Chelsea, Mreno, Mario Jose Dos Santos Ferlix Mourinho amemtuhumu
waziwazi kocha wa Tottenham Hospurs, Andre Villas-Boas kuwa aache tabia
ya kitoto baada ya kuanza vita ya maneno, lakini amekiri kuwa Spurs
msimu huu ni washindani wa kweli wa kombe la ligi kuu soka nchini
England.
Mournho
amejibu maneno ya Villas-Boas aliyekaririwa akisema kuwa kamwe hakosi
usingizi kuhusu Chelsea pamoja na uhusiano wake mbovu na kocha wake Jose
Mourinho.
AVB alisema kabla walikuwa na mahusiano mazuri na Mourinho, lakini yalishavunjika na haimpi shida.
“Haihitaji maelezo kuhusu urafiki na mahusiano yetu na yeye, yalivunjika kitambo”.
” Tunaheshimiana sana na hakuna jinsi, lazima tutaonana tu, lakini sijali kuhusu Chelsea na sio wajibu wangu”. Haya ni baadhi ya maneno ya AVB.
” Tunaheshimiana sana na hakuna jinsi, lazima tutaonana tu, lakini sijali kuhusu Chelsea na sio wajibu wangu”. Haya ni baadhi ya maneno ya AVB.
Leo
hii kocha mwenye jeuri ya maneno Jose Mourinho amesema: ‘Mimi sio mtoto
– kama nina tatizo na mtu yeyote namfuata tunazungumza na kuyamaliza”
Anahofu? Jose Mourinho amekiri kuwa Totenham watatoa changamoto kubwa ya ubingwa msimu huu
Kitu cha London: Jose Mourinho akiangalia mazoezi ya vijana wake kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Spurs
Mourinho aliuliza uhusiano wa Andre Villas-Boas’s na Sir Bobby Robson.
Robson
anasemekana aliingia katika mahusiano yasiyo mazuri na AVB baada ya
kocha huyo kumuingilia katika masuala ua upangaji wa timu katika klabu
ya Porto.
Lakini,
alipoulizwa kama mambo ya Robson yatakuwa na ushawishi katika mchezo wa
kesho katika dimba la White Hart Lane, Mourinho alisema: ‘Wapi Andre alifanya kazi na Bobby Robson? Niambieni – wapi, alifanya kazi naye?’
‘Namkumbuka mke wangu na watoto wangi kila wakati nikifika hapa asubuhi – hivyo ndivyo ilivyo.’
Wachezaji wenye ujuzi mkubwa: Oscar (katikati), Eden Hazard (kulia) na Samuel Eto’o wakiangaliwa na Mourinho
Hakuna mapenzo tena: Jose Mourinho (kushoto) na Andre Villas-Boas wameingia katika vita ya maneno
Mata anaweza: Mourinho amekiri kuvutiwa na kiwango cha Mhisapania huyo katika mchezo wa Capital One Cup
Wakati
huo huo , Mourinho anatarajia kumtumia Juan Mata katika dimba la White
Hart Lane kesho baada ya kuonesha kiwango cha hali ya juu dhidi ya
Swindon.
Kocha
wa Chelsea aliongeza: ‘Ana akili za kitaalamu na kimataifa. Amefanya
jitihada kubwa kunishawishi nimuamini. Kwahiyo sasa niko upande wake.’
RATIBA YA MECHI YA KESHO LIGI KUU SOKA NCHINI ENGLAND NI KAMA IFUATAVYO
28/09 04:45
|
Tottenham
|
- |
Chelsea
|
||||||
28/09 07:00
|
Manchester United
|
- |
West Bromwich Albion
|
||||||
28/09 07:00
|
Southampton
|
- |
Crystal Palace
|
||||||
28/09 07:00
|
Hull
|
- |
West Ham
|
||||||
28/09 07:00
|
Fulham
|
- |
Cardiff
|
||||||
28/09 07:00
|
Aston Villa
|
- |
Manchester City
|
||||||
28/09 09:30
|
Swansea
|
- |
Arsenal
|
0 comments:
Post a Comment