Mtaalamu
wa macho akimuhudumia mkazi wa Bagamoyo aliyejitokeza katika kambi ya
matibabu ya bure iliyofanyika jana Kerege Bagamoyo chini ya uratibu wa
Rotary Club Dar es salaam. Watu wote waliobainika na matatizo ya macho
walipatiwa miwani bure( picha zote na Ochieng Ogweno)
Mkurugenzi
wa huduma za miradi wa Rotary club Dar es salaam akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu kambi ya tatu ya matibabu ya bure
iliyofanyika kijiji cha Kerege Bagamoyo.
Mwenyekiti
wa Serikali ya kijiji cha Kerege ndg Haroub Boga akizungumza na
waandishi wa habari juu ya umuhimu wa kambi ya matibabu bure. Kulia,
mwenye bahasha ni Afisa Uhusiano wa Trinity Promotions, ambao pia
walikuwa wadhamini wa kambi hiyo bwana Ngwegwe Mussa.



Sehemu
ya watu waliojitokeza katika kambi ya matibabu ya bure katika kijiji
cha Kerege Bagamoyo. Kambi hiyo ni ya tatu kufanyika na zaidi ya watu
600 walijitokeza kupatiwa huduma mbalimbali ikiwemo kupatiwa miwani,
vyandarua na dawa bure.

Daktari
Jaynika Solanki akimpima shinikizo la damu Amina Salum (6) mkazi wa
kijiji ya Kerege Bagamoyo katika kambi ya matibabu ya bure iliyofanyika
jana kijiji Cha Kerege Bagamoyo

Rais
wa Klabu ya Rotary Dar es salaam Bi Nadine Atallah akizungumza na
waandishi wa habari jana katika kambi ya matibabu ya bure iliyoratibiwa
na Rotary Club Daressalaam
……………..
Klabu
ya Rotary Dar es Salaam Oysterbay kupitia miradi ya huduma
iliyotengenezwa kuimarisha miundombinu ya usafi na afya katika jamii,
inafanya shughuli mbili ambazo zinatarajiwa kuboresha maisha ya wakazi
wa wilaya ya Bagamayo kwa miaka ijayo.
Shughuli
ya kwanza kati ya hizo ni kukabidhi mradi kamili wa miundo mbinu ya
maji taka uliogharimu milioni 28 fedha za kitanzania hapo tarehe 14
Septemba 2013 na ya pili, tarehe 15 Septemba 2013 kutakuwa na kambi ya
matibabu ambapo wataalamu kadhaa wa afya wa kujitolea watawahudumia
zaidi ya wakazi 700 wa Bagamoyo kwa matatizo mbalimbali ya kiafya na
magonjwa.
MAKABIDHIANO YA MRADI WA USAFI
Klabu
ya Rotary ya Oysterbay imekarabati miundo mbinu ya maji taka katika
shule mbili za msingi Kerege na Mapinga, kwa kujenga vyoo vipya,
kuunganisha umeme, kuweka mabomba ya maji, mfumo wa usafishaji maji
unaoweza kuzalisha maji safi ya kunywa, n.k, vyenye jumla ya shilingi
milioni 28 fedha za kitanzania.
Makabidhiano
hayo yatafanyika katika kila shule na yanategemewa kuhudhuriwa na
wanafunzi, walimu, maafisa wa shule, viongozi wa mitaa na wana klabu wa
Rotary.
KAMBI YA MATIBABU
Kambi
ya matibabu, ambayo kwa sasa imekuwa ni tukio la kila mwaka, ipo katika
mwaka wake wa tatu na itafanyika Jumapili, Septemba 15. Wanataaluma na
wataalam wa tiba watawapima takribani watu 700 wenye magonjwa mbalimbali
yakiwemo malaria, upungufu wa damu, kisukari na shinikizo la damu na
kwa mara ya kwanza, watapima kansa ya kizazi. Pia upimaji wa hiari wa
virusi vya UKIMWI utakuwepo. Kambi ya mwaka huu itajikita katika kuzuia
malaria, elimu, matibabu, naiwapo akiba itaruhusu, vyandarua vya bure
vitatolewa kwa washiriki wa kambi. Kila mgonjwa atapatiwa taarifa za
jumla za kiafya zinazoonesha magonjwa mengine yaliyozoeleka na sababu
hatarishi. Ushauri nasaha utatolewa juu ya mienendo ya maisha kama vile
lishe na umuhimu wa mazoezi.
Zaidi
ya madaktari 50 na wafanyakazi wasaidiziwatakuwa wakisaidia katika
usajili, upimaji na ugawaji wa vyandarua. Vipimo vyote, ushauri nasaha,
na ushauri wa kitabibu utatolewa kwa wagonjwa bure. Rufaa kwenda
hospitali zitatolewa penye uhitaji wa kufanya hivyo.
“Lengo
la kambi ni kuleta huduma za msingi za afya zilizobora kwa watu ambao
vinginevyo wasingeweza kuzipata,” alisema Vikash Shah,mkurugenzi wa
kamati ya miradi ya huduma ya Klabu ya Rotary Dares Salaam Oysterbay.
Mradi
huu usingewezekana bila ya fedha zilizokusanywa katika kampeni ya
uchangishaji fedha ya Rotary Dar Marathon, klabu ya Rotary ya
Vancouver, na Rotary International zilizofanyika kwa njia ya Ruzuku
Linganishi.
“Tunafurahana
kujivunia kwamba kupitia jitihada za pamoja kati ya jamii, wana Rotary
wa kitaifa na kimataifa, taasisi zisizo za kiserikali, jamii ya kitabibu
na makampuni ya kibiashara; tumeweza kuandaa kambi hii ya matibabu kwa
mara ya tatu,” alisema Nadine Atallah, Raisi wa klabu ya Rotary Dar es
Salaam Oysterbay 2013-2014. Aliongeza kuwa,“mradi huu utafanyika pasipo
na vikwazo na tutaihudumia jamii zaidi na tunatazamia mafanikio kupitia
ushirikiano kwa miaka ijayo.”
Kambi
inaratibiwa kwa ushirikiano wa Shree Hindu Mandal Hospital kwa
kusaidiwa na KidzCare Tanzania, Sanitas Medical Centre, Tanzania Health
Promotions Support, The Tanzania Diabetes Association, ICAP,Sayona,
Trinity Promotions Ltd, Vesper Security, Knight Support, Aga Khan
Hospital, Aga Khan University, Jamana Printers, Supplies Stores &
Jai Ambe Balvi Padmavati na ELIMIKA.
Mbali
na hao, “Seattle4 Rotary Clubs” kutoka Seattle, Washington, USA ambao
wamechangia kwa kiasi kikubwa mradi wa upimaji wa malaria na vifaa
vitakavyokuwepo siku hiyo, pia watahudhuria.
HISTORIA
Kambi
ya kwanza ya matibabu ya bure ilifanywa na klabu mwaka 2011 katika eneo
la Chanika na zaidi ya watu 600 walipimwa malaria, virusi vya UKIMWI,
kisukari, magonjwa ya masikio,puana Koo (ENT), macho na dalili hatarishi
za magonjwa sugu. Dawa na miwani za bure zilitolewa kwa wale waliopimwa
na kugundulika na matatizo ya kiafya na matatizo ya kuona.Mwaka 2012
tulihudumia zaidi ya watu 700. Mwaka huu pia inategemewa idadi sawa ya
watu watasajiliwa kwa utaratibu wa kwanza kuja wa kwanza kudumiwa.
About Rotary
Rotary
Internatinal ni Shirika la kwanza duniani la klabu za huduma lenye
wananchama zaidi ya milion 1.2 katika vilabu 33,000 duniani kote.
Wanachama wa Rotary ni viongozi wa biashara wanaofanya kazi kitaifa,
kikanda na kimataifa kwajili ya kupambana na njaa, kuboresha afya na
usafi wa miundombinu ya majitaka, kutoa elimu, kuhamasisha amani na
kutokomeza polio. Kaulimbiu yetu ni “Huduma zaidi ya Binafsi”.
Klabu
ya Rotary Dar es Salaam Oysterbay inawakaribisha wanachama wapya. Kwa
maelezo zaidi kuhusu klabu, wanachama wake, na kazi za kijamii Tanzania
nzima, tembelea www.rotarydar.com.
0 comments:
Post a Comment