Mkurugenzi
wa Executive Solutions, Aggrey Marealle akizungumza na Waziri wa
Michezo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Banza Mukalayi kwenye mbio
za Kinshasa Marathon zilizoandaliwa na Executive Solutions.
Anayesikiliza ni John Addison, Mkurugenzi wa Wild Frontiers ya Afrika
Kusini.
Washiriki wa Kinshasa Marathon wakijiandaa kuanza mbio. Mbio hizo ziliandaliwa na Executive Solutions ya jijini Dar es salaam.
Mkuu
wa Alerte Rouge, Fanny Kazadi Nyembwe akimkabidhi zawadi Mutumbe Mande
ambaye aliibuka mshindi wa mshindi wa mbio za Kinshasa Marathon. Mbio
hizo ziliandaliwa na Executive Solutions ya jijini Dar es salaam.
Warembo
wakiwa wameshikilia mifano ya hundi kwa ajili ya kuwakabidhi washindi
wa Kinshasa Marathon. Mbio hizo ziliandaliwa na Executive Solutions ya
jijini Dar es salaam. Mwamvita
Makamba, Afisa wa Masuala ya Jamii kutoka Vodacom Afrika Kusini
akishiriki mbio za Kinshasa Marathon pamoja na Mdhamini wa Kampuni ya
Vodafone ya Uingereza Lord Michael Hastings.
Waandaaji
John Addison wa Wild Frontiers, Mwesiga Kyaruzi wa Executive Solutions
na Debbie Harrison wakiwa kwenye hafla fupi iliyofanyika baada ya mbio
za Kinshasa Marathon kumalizika.
…………..
Na Ibrahim Kyaruzi
Mbio
za Kinshasa Marathon zilizofanyika huko Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo
wiki hii imepata mafanikio makubwa baada ya kupata washiriki zaidi ya
5,000 idadi ambayo ni kubwa sana kwa marathon ya kwanza.Mbio hiyo
iliyodhaminiwa na Vodacom Congo imechangisha kiasi cha shilingi bilioni
1.6 ambazo zitatumika kusaidia watu walioathirika na vita kwenye mji wa
Goma uliopo Mashariki mwa nchi hiyo kupitia kampeni ya Alerte Rouge.
Meneja
Mradi wa Alerte Rouge wa Vodacom Congo, Fanny Kazadi Nyembwe
aliwashukuru waandaaji wa mbio hizo Executive Solutions ya Tanzania,
CMCT ya DRC, Wild Frontiers na Deep Blue Media za Afrika Kusini kwa
kufanya kazi kubwa sana kuifanya mbio hiyo ya kwanza jijini Kinshasa
kuwa yenye mafanikio makubwa.
“Sisi
Vodacom Vongo kupitia kampeni ya Alerte Rouge tumefurahishwa sana na
matokeo ya mbio hizi za Kinshasa Marathon kuweza kupata washiriki wengi
kuliko matarajio yetu. Executive Solutions pamoja na wadau wengine
wametusaidia sana kuifanya mbio hii iwe ya kiwango cha kimataifa na
kuweza kuvutia watu wengi ukizingatiia ni mara ya kwanza. Alerte Rouge
ni kampeni ambayo inaendeshwa na Vodacom Congo ili kusaidia watu wa Goma
ambao kwakweli wameathirika na vita hasa akina mama wajane na watoto
yatima. Tayari tumeishapeleka msaada wa chakula na sasa kutokana na
fedha hizi tulizopata kwenye mbio hii tutapeleka misaada ya mablanketi,
vyandarua, madawa pamoja na kuboresha huduma za afya.” Pia aliwashukuru
wakazi wa Kinshasa kwa muitikio mzuri na kujitokeza kwa wingi.
Aggrey
Marealle, Mkurugenzi wa Executive Solutions, waandaaji wa mbio hizo
alielezea kufurahishwa kwake na mbio hizo na kusema kuwapongeza
shirikisho la Riadha la DRC kwa kutoa ushirikiano mkubwa katika masuala
ya kiufundi ili kufanikisha mbio hizo.
“Ni
mafanikio makubwa sana kwa Kinshasa Marathon kuweza kuwa tukio kubwa la
namna hii ukizingatia ni mara ya kwanza jijini hapa. Kilimanjaro
Marathon ya kwanza ilipata washiriki 750 lakini Kinshasa Marathon ya
kwanza imepata washiriki zaidi ya 5,000 na tumefanya maandalizi katika
muda wa mwezi mmoja na nusu muda ambao ni mfupi ukilinganisha na
Kilimanjaro Marathon ambapo huwa tunafanya maandalizi kwa muda
usiopungua miezi sita.”
Marealle
alisema kuwa hii inamaanisha kuwa wananchi wa Kinshasa wameguswa na
matatizo yanayowakabili wenzao walioko Goma. na Tutanya mbio nyingine
kwenye miji ya Lubumbashi, Kisangani na Goma katika miezi ijayo na
tunaamini kuwa watu watazidi kujitokeza hivyo tunawaomba pia Watanzania
kujitokeza kwa wingi kushiriki.
Naye
Mkurugenzi wa Wild Frontiers Joh Addison aliyaomba makampuni mbalimbali
katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na Afrika nzima kwa ujumla
kujitokeza kushiriki katika mbio zijazo ili kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na Vodacom kupitia kampeni ya Alerte Rouge.
0 comments:
Post a Comment