- MAELFU YA WATU WAFURIKA KUMSIKILIZA KATIBU MKUU
- VIONGOZI 43 KUTOKA UPINZANI WARUDISHA KADI
- WANACHAMA 126 WAJIUNGA HAPO HAPO
Mbunge
wa Rorya Ndugu Lameck Okambo Airo akihutubia wakazi wa Shiratu
waliofurika kwenye uwanja wa Shiratu Obwere jana,Mbunge huyo alieleza
jinsi gani amefanikiwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.(PICHA NA
ADAM MZEE NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-SHIRATI RORYA)
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Geita Ndugu Joseph Musukuma akiwasalimu wakazi wa
Shiratu ,na kuwapongeza wananchi wa wilaya ya Rorya kwa umoja na
mshikamano walio nao.
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Wanawake nchini Ndugu Amina Makilagi akihutubia wakazi
wa Shiratu kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni Rasmi alikuwa Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Shiratu
wilaya ya Rorya na kuwataka wananchi hao kuwapuuza wanaotaka kuharibu
mchakato wa kupata Katiba Mpya kwani Mchakato wa Katiba hiyo imefuata
taratibu zote za kisheria.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Shiratu
kwenye viwanja vya Shiratu Obwere na kuwaambia wakazi wa Shiratu kuwa
CCM inatekeleza ahadi zake ilizoahidi kwa wakazi wa wilaya ya Rorya
,Katibu Mkuu aliwaeleza wananchi hao mipango iliyofanyika na
itakayofanyika kwa ajili ya maendeleo ya wilaya hiyo,hasa katika suala
zima la mradi wa umeme vijijini,maji,shule na huduma za afya.
0 comments:
Post a Comment