KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amewataka wawekezaji nchi
kujenga tabia ya kutoa michango ya maendeleo kwenye maeneo ambayo
wamewekeza na si kutoa michango ili kumfurahisha Rais au Waziri Mkuu.
Kinana
alitoa kauli hiyo jana katika Kijiji cha Mwendakulima katika Wilaya ya
Kahama mkoani Shinyanga ikiwa ni siku yake ya kwanza ya ziara yake
ambayo itakuwa kwa Mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara ambapo akiwa eneo
hilo alizungumzia umuhimu wa wawezaji kujitahidi kufanya maendeleo kwa
wananchi ambao wamewekeza kwenye maeneo yao.
“Wawekezaji
wapo tayari kutoa hadi sh.milioni 200 wakiwa Dar es Salaam, Mwanza au
Arusha, lakini ushauri wangu kwao, ni vema wakachangia kwenye maeneo
ambayo wamewekeza kwani hiyo itasaidia kuondoa malalamiko lakini pia
itakuwa ni jambo jema wananchi kunufaika kutokana na uwekezaji huo.
Alisisitiza
kuwa anatambua umuhimu wa wawekezaji kuchangia maendeleo lakini
inapendeza zaidi inapofika mahali wananchi wakawa na maendeleo kutokana
na wawekezaji.
Kinana
alifafanua hayo zaidi wakati akizindua kituo cha afya kwenye kijiji
hicho ambacho kimejengwa na kampuni ya madini ya Buzwagyi ambapo alisema
kampuni hiyo imeanza na eneo la afya lakini mwaka mwingine wanaweza
kujenga miundombinu ya barabara na mwaka unaofuata kufanya jambo lingine
la maendeleo.
Wakati
huo huo Katibu Mkuu huyo , alisema kuwa Watanzania wanatakiwa kushiriki
kikamilifu kwenye mchakato wa Katiba mpya na kwamba msimamo wa chama
chake ni Serikali mbili lakini wapo tayari kwa uamuzi ambao utafanywa na
wananchi kwa kuamua aina ya katiba ambayo wanahitaji.
Pia
alisema wananchi wafahamu kuwa licha ya umuhimu wa kuwa na Katiba mpya
lakini hiyo haitakuwa mbadala wa kuwa na mabadiliko ya maisha baada ya
kupatikana kwake ambapo alitoa mifano ya nchi kadhaa Afrika na Asia
ambazo zilipata katiba mpya lakini hali ya uchumi kwa watu wake imebaki
kuwa ile ile.
Akifafanua kuhusu msimamo wa CCM wa kutaka muundo wa Serikali mbili, Kinana alisema hakuna
sababu ya kuwa na Serikali ya tatu kwani kuwanayo ni kuongeza mizigo kwa Mtanzania kwani ni gharama kuindesha kwake lakini pia haitakuwa na kazi.
sababu ya kuwa na Serikali ya tatu kwani kuwanayo ni kuongeza mizigo kwa Mtanzania kwani ni gharama kuindesha kwake lakini pia haitakuwa na kazi.
Pia Kinana akiwa Kahama alizindua Saccos ya Mkombozi katika eneo la Isaka ambapo alitumia
nafasi hiyo kuwahimiza wananchi kubuni miradi ya maendeleo lakini pia kwa vijana kujiendeleza kielimu hasa kusoma masomo ya ufundi yakiwamo ya ujenzi, ufundi mchundo na aina nyingine nyingine ya taaluma ya ufundi ambayo
itawawezesha kupaa kipato.
nafasi hiyo kuwahimiza wananchi kubuni miradi ya maendeleo lakini pia kwa vijana kujiendeleza kielimu hasa kusoma masomo ya ufundi yakiwamo ya ujenzi, ufundi mchundo na aina nyingine nyingine ya taaluma ya ufundi ambayo
itawawezesha kupaa kipato.
Katika
kuhakikisha hilo la masomo ya ufundi linafanikiwa,Kinana aliweza kutoa
ahadi ya kusomesha vijana 10 wa eneo la Kahama na kwamba kama gharama
itakuwa nafuu ataongeza idadi ya vijana ikiwa ni sehemu ya kufanikisha
malengo ya vijana.
Wakati
huo huo akiwa katika Uwanja wa CDT Kinana aliwataka Watanzania kuwa
makini na wapinzani kwani nia yao si kuwaisaidia Watanzania bali n
kutafuta maslahi yao na ndio maana wapo tayari kufanya lolote
kufanikisha kile wanachokitaka.
0 comments:
Post a Comment