Monday, September 9, 2013


Kiggi1 

Na  Baraka Mpenja, Mbeya
KUFUATIA maneno ya hapa na pale kuibuka na kuushutumu uongozi wa Simba kuwa wamechelewa kumtibu goti winga wake, Kiggi Makassi na kuonekana kama hawajali wanandinga wake, hatimaye ukimya wavunjwa na sasa safari imeiva, huku maandalizi yote yakikamilika.
 Kwa taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa, Kiggi  anaondoka leo kuelekea nchini India kwa matibabu ya goti lake.
Afisa habari wa klabu ya Simba, Ezekiel Kamwaga kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Facebook, amesema Makassi anaondoka leo saa 10:45 jioni kwa ndege.
Kamwaga amesema kila kitu kipo sawa na kwa sasa Makassi ndio anaelekea uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam tayari kwa safari hiyo.
Nyota huyo aliyesainishwaa na Simba akitokea kwa wapinzani wao wa jadi, klabu ya Yanga, anaendea kufanyiwa upasuaji wa goti ambalo limemuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
“Tumwombee Kiggi kwani oparesheni ya goti ni ngumu sana, hivyo Watanzania kwa ujumla, mashabiki na wanachama wa Simba waombe dua njema kwa kijana wao”. Alisema Kamwaga.
Siku za nyuma Kiggi aliwahi kutajwa kwenda kwa mganga wa jadi kwenda kutibu goti lake kwa madai kuwa viongozi wa Simba bado hawajaamua kumpeleka katika matibabu bora, lakini uongozi wa Simba kupitia kwa mwenyekiti wake, Alhaj Ismail Aden Rage ulisema kuwa unajiandaa kumpeleka India na kusema kuwa mchezaji hapelekwi huko kama anapelekwa sokoni.
“Unapompeleka mchezaji India lazima uwa na miadi na madaktari wa huko, huwezi kumpeleka kama wampeleka sokoni bwana.. lazima mjue, Simba tunajiandaa na kuwasiliana na wenzetu wa India, itafika wakati lazima ataondoka”. Alikaririwa Rage.
Sasa yametimia na safari ya nyota huyo imeiva na leo hii anakwea pipa.
Dawati la michezo mtandao wa MATUKIO DUNAINI linamtakia kila la heri Kiggi Makassi katika safari yake ya India na Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema amsaidie katika upasuaji wake ili arejee uwanjani na mashabiki waendele kupata raha kutoka kwake.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video