Hatua hii ni kutokana na ombi la serikali ya Kenya kwa Interpol.
Bi
Lewthwaite, mwenye umri wa miaka 29, ni mjane wa mlipuaji aliyefanya
shambulizi la kujitoa mhanga mjini London Uingereza mwezi Julai mwaka
2005
Anajulikana kama “white widow”, na amehusishwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab nchini Somalia.
Polisi
wa Interpol hata hivyo hawakuhusisha hatua ya kumsaka Samantha na
shambulizi la kigaidi dhidi ya jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi
lililowaua watu 67.
Hata hivyo, hatua hii ya kumsaka Bi Lewthwaite inakuja punde baada ya shambulizi hili la kigaidi nchini Kenya.
Al-Shabab
ilikiri kufanya mashambulizi hayo yaliyotokana na kutekwa kwa jengo la
Westgate na kisha kutekwa kwa raia wa kawaida waliokuwa ndani ya jengo
hilo kwa siku nne.
Kwa
mujibu wa polisi wa Interpol, mwanamke huyo anasakwa na serikali ya
Kenya kwa kumiliki mabomu na kupanga njama ya kufanya mashambulizi
kuanzia Disemba mwaka 2011.
Ikiwa
mwanamke huyo atakamatwa katika nchi mwanachama wa Interpol, atazuiliwa
na kusibiri kupelekwa katika nchi anayotakikana kwa kesi kufunguliwa
dhidi yake.
Bi
Lewthwaite anajulikana kwa jina bandia la, “Natalie Webb” –na alikuwa
anasakwa kwa madai ya kumiliki hati bandia ya usafiri nchini Afrika
Kusini.
Ni
mjane wa Germaine Lindsay, mmoja wa washambuliaji wanne waliohusika na
shambulizi la kigaidi mjini London ambapo watu 52 waliuawa na mamia ya
wengine kujeruhiwa.
CHANZO: BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment