Na Baraka Mpenja , Mbeya
KIUNGO
wa zamani wa klabu ya Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa stars
aliyetoroka kambini mwezi julai mwaka huu wakati Stars ikijiandaa na
mechi ya kuwania kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Uganda `The Cranes`
katika uwanja wa Namboole Kampala, Mwinyi Kazimoto Mwitula ametuma
salamu za shukurani kwa mashabiki wa Simba, viongozi na watanzania wote
waliokuwa wanamuunga mkono.
Ujumbe
ambao Kazimoto ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa
Facebook maarufu kwa jina la FB amesomeka kama ifuatavyo;
“Najua
sikupata muda wa kuwashukuru watanzania wote waliokua wananiunga mkono
kwa support yao siku zote kwanza,, haswa haswa wapenzi wa
simba,viongozi,wanachama kwa kunivumilia kwa mabaya na mazuri
yote,,,nawatakia simba mafanikio mema kwenye ligi……pamoja sana…”.
Jembe
la kazi!: Kazimoto Alitoroka kambi ya timu ya Taifa, Taifa Stars akiwa
jijini Mwanza kujiandaa na mchezo dhidi ya Uganda, lakini aliomba radhi
na yakaisha. Sasa anag`ara huko Qatar.
Ikumbukwe
kuwa Kitendo alichokifanya nyota huyu kutoroka katika kambi ya Taifa
kilitafsiriwa kuwa ni kukosa uzalendo kwani Stars ilikuwa inakabiliwa na
mchezo mgumu zaidi.
Kocha
wa Taifa Stars, Kim Poulsen alisikitishwa sana na kitendo alichofanyiwa
na kiungo wake tegemeo katika kikosi chake, lakini baadaye zilitoka
taarifa kuwa ametimkia Qatar kwenda kucheza soka la kulipwa na kim
kubariki mafanikio ya nyota wake.
Mkali wa kumiliki gozi na kupiga pasi za uhakika: Mwinyi kazimoto enza zake akiwa Simba kuonesha maujuzi ya hali ya juu
Baadaye
Kazimoto alijitokeza na kuandika barua ya wazi akiwaomba radhi
watanzania, shirikisho la soka Tanzania, TFF, Uongozi wa Simba kwa
kitendo alichofanya.
Kazimoto
alieleza kuwa siku zote alikuwa ana ndoto ya kucheza soka la kulipwa,
hivyo baada ya kupata timu Qatar alishawishika kutoroka kwani nafasi
ilikuwa adimu na ya haraka kwake. Lakini baadaye kuna taarifa zilitoka
kuwa alitoroka kwasababu kuna baadhi ya watu walimkera.
Kazimoto
ambaye kabla ya kujiunga na Simba, alikuwa anakipiga kwa maafande wa
Jeshi la kujenga Taifa, JKT Ruvu kutoka mwaka 2007-2011 na akajiunga na
wekundu wa Msimbazi Simba mwaka 2011 na kuwa kiungo tegemeo mpaka
anaondoka mwaka katikati ya mwaka huu.
Kijana
huyo anawavutia wapenzi wengi wa soka kwa uwezo wake wa kupiga mashuti
na kufunga mabao ya mbali, lakini pia kumiliki mpira na kupiga pasi za
uhakika.
Kwa sasa nyota huyo mzaliwa wa mwaka 1988 mjini Dodoma anakipiga huko nchini Qatar katika klabu ya Al Markhiya.
Wakati
huo huo, nahodha wa mabingwa watetezo wa ligi kuu soka Tanzania bara,
Nadir Haroub `Canavaro` amefurahishwa na kitendo cha uongozi wa timu
yake chini ya mwenyekiti Yusuf Manji kumaliza sakata la Mrisho Ngassa
kwa kukubali kulipa deni la milioni 45 kwa klabu ya Simba SC na kutoa
kauli kuwa sasa kesho ndio wanaanza ligi dhidi ya Ruvu Shooting.
Canavaro
ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook ambao
mara nyingi huwa anautumia kutoa kauli tofauti kwa mashabiki wake kuwa;
“Habari’ Mwenyekiti kayamaliza..kesho tunaanza kazi…. #yangadaimambele”
Ujumbe
huu hauko moja kwa moja, lakini kutokana na sakata la Ngassa kuwa
habari ya mjini kwa sasa na uongozi kukubali kulipa deni lake na kusema
kuwa nyota huyo atacheza kesho, inatosha kujiridhisha kuwa Canavaro
anamaanisha urejeo wa nyota huyo baada ya kifungo cha mechi 6.
Wakati
hayo yakijiri, naye kocha msaidizi wa Yanga, Fred Ferlix Minziro
amekaririrwa na vyombo vya habari akisema kuwa kesho Ngassa atakuwa
miongoni mwa wachezaji 11 watakaoanza katika kikosi cha kocha Ernie
Brandts dhidi ya Ruvu Shooting katika dimba la Taifa jijini Dar es
salaam.
0 comments:
Post a Comment