Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akiwapa
nasaha wanamichezo wa wizara hiyo katika tafrija fupi ya kuwaaga
wawakilishi wa wizara hiyo ambao watashiriki katika mashindano ya
Shirikisho ya Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (Shimiwi)
yatakayofanyika mjini Dodoma Jumamosi. Tafrija ya kuwaaga wanamichezo
hao ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Maafisa wa Polisi
jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wa nne
kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wanamichezo wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kuwaaaga rasmi katika tafrija
iliyofanyika Chuo cha Maafisa wa Polisi, jijini Dar es Salaam leo.
Abdulwakil aliwataka wanamichezo hao wahakikishe wanashirikiana ipasavyo
na hatimaye wanashinda michezo aina mbalimbali inayotarajiwa kuanza
mjini Dodoma Jumamosi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
0 comments:
Post a Comment