Wakenya walimaliza siku tatu za maombolezi Ijumaa.
Imetimia juma moja kamili tangu jengo la maduka mjini Nairobi kushambuliwa na watu wengi kuuwawa.
Watu
wenye silaha walivamia jengo la Westgate, magharibi mwa Nairobi, na kwa
siku kadha waliendeshana mbiyo na vikosi vya usalama huku wakifyatua
risasi na kuuwa wateja waliokuwamo kwenye maduka hayo, pamoja na watoto.
Hadi sasa inajulikana kuwa watu 67 waliuwawa.
Mamia ya watu walikuwemo kwenye jengo la biashara washambuliaji walipoanza uvamizi Jumamosi iliyopita.
Mwandishi wetu mjini Nairobi anasema moto bado unatokota sehemu ya jengo hilo.
Alama za risasi zinaonekana kwenye kuta – matokeo ya mapambano baina ya jeshi la Kenya na wapiganaji.
Zana
nzito zinatumiwa kunyanyua kifusi cha saruji, na hapo ndipo itajulikana
iwapo washambuliaji waliuwawa na mateka wangapi zaidi walikufa
CHANZO: BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment