Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
HATIMAYE Gareth Bale amekamilisha uhamisho wake jana usiku kujiunga na Real Madrid kwa dau nono la pauni milioni 86 na kuvunja rekodi ya pauni milioni 80 ya Cristiano Ronaldo wakati ule akiunga na klabu hiyo mwaka 2009.
Baada ya makubaliano, Bale atalipwa pauni laki 2 na elfu 56 kwa wiki, na ameanguka mkataba wa miaka 6 na leo hii jumatatu anatarajiwa kupima afya yake tayari kwa kazi moja ya kuing`arisha Real Madrid na kutambulishwa kwa waandishi wa habari.
Sasa Bale amekuwa mchezaji ghali zaidi duniani baada ya kupiku rekodi ya Ronaldo, na kilichobaki kwake ni kuonesha kuwa ana uwezo mkubwa na analingana na dau kubwa kiasi hicho.



0 comments:
Post a Comment