Wataalam
kutoka Idara ya Afya Wilaya ya Mpanda wakiongozwa na Mratibu wazee
Mwenye Kofia Dr, Patrick Mwita wakati wakiwa nyumbani kwa Bibi Kizee
ambaye hata jina lake halikuweza kufahamika kwa kuwa hawezi hata kuongea
wataalamu hao walikuwa wakimwangalia Bibi Kizee huyo mwenye umri
unaokadiliwa kuwa zaidi ya miaka mia moja katika kijiji cha Dirifu Kata
ya Machimboni Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi anayeishi pekee yake
bila msaada wowote.wataalam hao walikuwa katika zoezi la kuwatambua
wazee wenye umri kuanzia miaka siti na kuendelea ili wapatiwe
vitambulisho vya matibabu vya bima ya Afya vitakavyowasaidia kupatia
huduma ya matibabu bure kwenye hospitali
Wakazi
wa Mwambao wa Ziwa Tanganyika Kata ya Ikola wakiwa katika harakati za
maisha hapa wanaonekana baadhi ya akina mama na watoto wakifua nguo
wengine kuchota maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na wengine,
kuosha vyombo, wengine wakioga kwa pembeni na wengine kuendelea na
shughuli zao za kimaisha maadamu maisha yanaendelea bila kujari ya
Afya zao au hali yeyote inayoweza kuwapata hususani mlipuko wa magonjwa
yanayotokana na matumizi ya maji machafu kama hayo kwa wengine
wanajisaidia vichakani pembezoni mwa ziwa kwa kuwa desturi ya wakazi wa
mwambao wa ziwa hawana utamaduni wa kutumia vyoo..
Suala
la usafiri kwa baadhi ya maeneo hapa nchi bado ni changamoto ambayo
inatakiwa ipewe umuhimu na kipaumbele cha kipekee na mamlaka husika kama
inavyoonekana kwa wakazi hawa wa kijiji cha Itunya Kata ya Kapalamsenga
Wilayani Mpanda Wakivuka Mto unaotenganisha maeneo ya Kijiji cha
jirani cha Itunya na Kijiji cha Kapalamsenga daraja hilo ni la miti
lililotengenezwa na wananchi wenyewe bila msaada wowote wa
wataalamu.Jambo ambalo ni hatari kwa wakazi hao wakati wowote linaweza
kuleta madhara hapa watalaam kutoka Halmashauri ya wilaya ya Mpanda
wamefika kujionea na kushuhudia namna wananchi wanavyopata shubiri ya
usafiri hasa suala la kivuko ambacho hakina ubora kwa watumiaji kazi
kweliwekili miaka zaidi ya hamsini ya uhuru mambo bado ya Ujima.
(Picha zote na Kibada Kibada)
0 comments:
Post a Comment