Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi Sihaba Nkinga
(katikati) ambaye pia ni mgeni rasmi kwenye hafla ya kuiaga timu ya
Wizara akiwasili Uwanja wa Taifa huku akiwa amesindikizwa na Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa
Elisante Ole Gabriel (kulia) pamoja na viongozi wengine kushiriki hafla
ya kuwaaga wanamichezo wa SHIMIWI leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Msaidizi Utawala Bw. Titus Mkapa akitoa maelezo machache kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi kwenye hafla ya kuiaga timu ya Wizara
inayakwenda kwenye mashindano ya SHIMIWI jijini Dodoma, hafla hiyo
imefanyika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi Sihaba Nkinga
(kulia) akiwaasa wanamichezo wa timu ya Wizara kuzingatia maadili na
nidhamu katika michezo wanayokwenda kushiriki mjini Dodoma.
Bi.
Magreth Mtaki akisoma risala mbele ya mgeni rasmi wakati wa hafla ya
kuiaga timu ya Wizara inayoshiriki kwenye michezo ya SHIMIWI leo jijini
Dar es Salaam.
Baadhi
ya watendaji Wakuu wa Wizara ya Habari pamoja na asasi zake
wakimsikiliza Katibu Mkuu wakati akihutubia kwenye hafla ya kuiaga timu
ya Wizara inayoshiriki kwenye michezo ya SHIMIWI leo jijini Dar es
Salaam.
Bi. Magreth Mtaki akionyesha zawadi ya fedha taslimu kwa washindi walioshinda michezo ya SHIMIWI mwaka uliopita.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi Sihaba Nkinga
(katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa Wizara. Watatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO, DAR ES SALAAM.
0 comments:
Post a Comment