Wednesday, September 4, 2013


Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Mbeya
WAGOSI wa kaya, Coastal Union wenye makazi yao CCM Mkwakwani Mkoani Tanga “Waja leo waondoka leo” wemesema kukamilika kwa idara zote za kikosi chao ndio sababu ya wao kuwa  na majigambo makubwa mbele ya timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara.
Akizungumza na mtandao wa MATUKIO DUNIANI, Afisa habari wa klabu hiyo ambaye pia ni mchambuzi mzuri wa soka nchini, Edo Kumwembe amesema kuna timu zinamtia wasiwasi kwa kuanza vibaya, hivyo zinahitaji kujipanga vizuri kabla ya kukumbwa na balaa, lakini kwa upande wao mambo ni “supa”.
Kumwembe alisema kuna timu zimepanda ligi kuu  na kuanza vizuri huku akitaja klabu ya Mbeya City, lakini kwa Ashanti United amekiri hawajapanda na nguvu, na Rhino Rangers walikuwa na ratiba ngumu ya nyumbani dhidi ya Simba na Azam fc, hivyo walijitahidi na watapumua mechi zijazo.
“Lakini kinachonitia wasiwasi, kuna timu zilikaribia kushuka daraja kama Tanzania Prisons, ila hawajaja na jipya kwani wamepoteza mechi mbili, hivyo wanahitaji kujianga vizuri”. Alisema Kumwembe.
1Kikosi cha wagosi wa Kaya, Coastal Union (picha zote kwa hisani ya Coastal Union Blog)
Kwa upande wa timu za juu, Yanga, Simba na Azam FC, Kumwembe amesema bado hazijatulia sana lakini katika raundi ya tano au sita zitakuwa sawa zaidi, lakini kwa kuwa na pointi 4 kila mmoja ni dalili ya kujiandaa vizuri, ingawa bado hazina cheche kali.
Lakini kwa kikosi cha Wagosi wa Kaya, Kumwembe amesema katika misimu miwili iliyopita wameibadilisha timu yao na sasa imekuwa bora zaidi ya siku za nyuma, hivyo wanapojitapa kutwaa ubingwa wanajiamini.
“Mbali na kuwa na kikosi bora, bado tunaye mwalimu bora zaidi, Hemed Morroco amekamilika kufundisha soka, ukiangalia vikosi vya timu nyingine ingawa vina majina makubwa ni vya kawaida sana, ila wagosi wa Kaya wamekamilika”. Alijitapa Kumbwembe
IMG_7149Kumwembe amesema idara zote ziko sawa, langoni kuna kipa bora, Shaaban Kado, safu ya ulinzi kuna wachezaji wazuri wakiwemo Hamad Juma, Abdi Banda, Marcus Ndehele, na Juma Nyoso.
Pia alisifu safu yao ya kiungo inayoongozwa na Razak Khalfan, Haruna Moshi “Boban”, Jerry Santo, Uhuru seleman, huku safu ya ushambuliaji ikiwa bora zaidi ikiongozwa na Mganda, Kato Yayo, Crispian Odula na Suleiman Kassim “Selembe”.
Kwa sasa Kumwembe amesema hesabu zao ziko katika mchezo ujao dhidi ya Tanzania Prisons katika uwanja wao wa nyumbani wa CCM Mkwakwani jijini Tanga, hivyo wanaendelea na mazoezi yao na wana uhakika wa kushinda.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video