Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Prof. Costa Mahalu akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kozi mpya ya kuwanoa watetezi wa haki za binadamu katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojulikana kwa jina la ‘Akiba Uhaki’, iliyofanyika Kawe Beach jijini Dar es
Salaam juzi. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila, Mkuu wa
kitivo cha Sheria cha Chuo hicho, Dk. Natujwa Mvungi na Mratibu wa Programu ya
taasisi ya Akiba Uhaki, Kepta Ombati.
Mkuu
wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila ambaye alikuwa mgeni rasmi
akizungumza katika hafla uzinduzi wa kozi mpya ya watetezi wa haki za
binadamu katika nchi za Afrika Mashariki.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Prof. Costa Mahalu (wa pili kulia), Mkuu
wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitivo cha
Sheria cha Chuo hicho, Dk. Natujwa Mvungi (kuli) na Mratibu wa Programu
ya taasisi ya Akiba Uhaki, Kepta Ombati. (kushoto).
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Prof. Costa Mahalu (kulia),wa pili
kulia ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo hicho, Dk. Sengondo Mvungi,
mwanafunzi wa chuio hicho, Hapiness Katabazi na mtangazaji wa Kituo cha
Televisheni cha Channel Ten, Salum Mkambala.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila akimpongeza mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Jane Kacuculi kutoka Uganda, ambaye amepata udhamini wa kusoma katika Chuo hicho kutoka katika taasisi ya kiraia ya Haki Uhaki ya nchini Kenya.
DAR ES SALAAM, Tanzania
SERIKALI imekipongeza Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), kwa uamuzi wake wa kuanzisha kozi ya kuwanoa watu wanaojitambulisha kuwa wao ni watetezi wa haki za binadamu katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwasababu kozi hiyo itasaidia watetezi wa haki za binadamu kufahamu wanachokifanya katika jamii.
Hayo
yalisemwa juzi usiku na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mercy Sila kwaniaba
ya Mkuu wa Pwani, Mwantumu Mahiza katika hafla ya chakula cha jioni
iliyofanyika katika chuo kikuu cha Bagamoyo Kawe Beach jiiini Dar es
Salaam, wakati akizindua rasmi program hiyo ya mafunzo ambayo imepewa
jina la’ Akiba uhaki’ ambapo inakuwa ni ya kwanza kutolewa hapa nchini.
Sila
alisema programu hiyo inaendeshwa na Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) na
kufadhiliwa taasisi ya kiraia ya Haki Uhaki yenye makao makuu yake
nchini Kenya, tayari imeishapata wanafunzi kumi toka nchi za
Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi na kwamba masomo hayo yatakuwa
yakitolewa kwa miezi sita na kuwataka wale wote wanaojiita wanaharakati
hapa nchini wafike katika chuo hicho ili waweze kufundishwa kwanza jinsi
ya kufahamu haki za binadamu ni zipi, na haki za kijamii ni zipi na hao
wanadamu wanatakiwa wazitii sheria za nchi wakati wakizidai hizo haki
zao bila shuruti.
“Tumeona
katika mataifa ya wenzetu vurugu kila kukicha na hata hapa nchini kuna
baadhi ya watu wanaojiita ni watetezi wa haki za binadamu na wamekuwa
wakitumia kinga hiyo kupotosha ukweli wa mambo ambayo yanafanywa na
serikali zao kwa kisingizio kuwa wa ni watetezi wa haki za binadamu
wakati hata elimu ya kutetea hizo haki za binadamu hawana …leo serikali
inapenda kupongeza program hii kwani itasaidia sana kuondoa mivutano na
malumbano baina ya watetezi wa haki za binadamu na serikali kwani mtu
atakayepata elimu hii atakuwa ameelimika na kufahamu haki za binadamu
zinapaswa zidaiwe kwa kutumia amani”alisema Sila.
Kwa
upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Profesa Costa Ricky
Mahalu aliishukuru serikali kwa kukubali kuja kuzindua program hiyo
kwani programu ni yakwanza kutolewa katika vyuo vya hapa nchini na
program hiyo itawezesha kuondoa malumbano baina ya serikali na watetezi
wa haki za binadamu kwani ni wazi hivi sasa kumeibuka watu
wanaojitambulisha kuwa ni watetezi wa haki za binadamu wakati hawana
hata elimu ya huo utetezi wa haki za binadamu na wamekuwa wakitoa baadhi
ya matamko ambayo hayana mantiki katika suala zima la utetezi wa haki
za binadamu hali ambayo alisema ikiachwa iendelee italeta madhara katika
jamii.
“UB
inaamini katika elimu zaidi…hivyo UB imeona ni jambo jema kuanzisha
program hiyo ya mafunzo ya muda mfupi kwa wale wote wanaotaka na
wanajiita watetezi wa haki za binadamu waje kufundishwa masuala hayo na
waadhiri waliobobea katika eneo hilo la masuala ya haki za
binadamu”alisema Profesa Mahalu.
Kwa
upande wake Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dk.
Natujwa Mvungi ambayo program hiyo ya Akiba uhaki inatolewa chini ya
kitivo chake alisema jumla ya wanafunzi 10 toka katika nchi tano za
jumuiya ya Afrika Mashariki wa kozi ya Akiba Uhaki ,wameishafika hapa
nchini na wanaanza mafunzo hayo kwa muda wa miezi sita kuanzia wiki hii
chuo hapo na kwamba wanafunzi hao wamefadhiliwa ada ya kusoma kozi hiyo
na taasisi isiyo ya kiserikali yenye makao makuu yake nchini Kenya ya
Akiba uhaki na kuwataka wale wote wanaojiita ni watetezi wa haki za
binadamu wakati hawana elimu ya kuonyesha wamefudhu kozi hiyo,wasisite
kuja kupata elimu hiyo chuo hapo.
0 comments:
Post a Comment