NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
CHAMA
cha kutetea abiria Tanzania(CHAKUA) kimezishauri kampuni za
usafirishaji zianzishe mfumo wa kukata tiketi kwa njia ya mtandao ili
kuweza kuepusha usumbufu kwa abiria kutokana na wapiga debe, vishoka,
wizi na tiketi feki kwa mabasi yaendayo mkoani.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari- MAELEZO kwa
niaba ya Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa chama hicho, Modesti
Mfilinge, mjumbe wa bodi hiyo, Renatus Kapira alisema utaratibu huo
utasaidia kupunguza tatizo la upandishaji nauli kiholela.
“Mfumo
huo utasaidia kuwatambua kwa urahisi abiria wote waliokuwemo kwenye
chombo husika pale inapotokea bahati mbaya wakapata ajali au au chombo
kuharibika ili waweze kurudishiwa gharama na kulipwa fidia.
Chama
hicho kimeishauri Serikali iangalie njia mbadala ya kuwasaidia abiria
watakaokuwa wanatoka mbali kufuata vituo kwa mfano wanaotoka
Mbagala,Kongowe au Chamanzi na maeneo mengine ya mbali kutuata basi la
Arusha au Tanga, ambapo mtu mwenye familia hulazimika kutumia Sh. 50,000
hadi Mbezi ya Kimara.
Aliongeza kuwa abiria wanaotoka maeneo hayo wanapata usumbufu kwa kuwa hakuna daladala zinatoka huko hadi katika kituo hicho.
Kapira
aliishauri Serikali kuwa iboreshe miundombinu katikavituo vya mabasi
yanendayo mikoani ili kuwezesha abiria wanasubiri kusafiri kesho yake.
Aidha
chama hicho kiliiomba Serikali kupitia vyombo vya usalama na mamlaka
nyingine kufanya ukaguzi kwenye mabasi yanayosafirisha abiria mikoani
kuwa ni si mabovu ili kuepusha ajali na usumbufu abiria.
0 comments:
Post a Comment