Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
NYOTA
wa zamani wa Brazil, Roberto Carlos ameonya kuwa mshambuliaji mpya wa
klabu ya Chelsea, Samuel Eto’o anaweza kuwa chanzo cha matatizo katika
chumba cha kuvalia nguo klabuni hapo.
Mkurugenzi huyo wa zamani
Anzhi Makhachkala amesema nyota huyo raia wa Cameroon alikuwa
anaingilia kazi zake wakiwa wote nchini Urusi mpaka ikafika wakati
akafikiria kuondoka.
Mwaka 2011, Carlos alikuwepo
Anzhi na alishawishi dili la kumnunua Eto’o kutoka Inter Milan, na
kumuweka kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi ulimwengu wa soka.
Onyo:
Roberto Carlos (chini), aliyekuwa mkurugenzi wa timu ya Anzhi, amesema
mchezaji mpya wa Chelsea Samuel Eto’o alikuwa chanzo cha kuharibiki
katika klabu yake ya zamani
Baada ya kufunga mabao 36 katika mechi 71, Eto’o
amejiunga na Chelsea kwa uhamisho wa bure majira ya kiangazi mwaka huu
na anaweza kucheza kwa mara ya kwanza jumamosi ya wiki hii dhidi ya
Everton.
Lakini katika mahojiano na gazeti la Globo, Carlos ameeleza kukatishwa tamaa kwa kile ambaco Eto’o alichangia wakati akiwa Anzhi.
Alisema: ‘Namjua Eto’o tangu nikiwa na miaka 16, na kutoka muda ule amekuwa mtu mzuri ambaye nampenda sana”.
‘Ni mtu mzuri, lakini kuna baadhi ya mambo nadhani huwa anakuwa chanzo cha matatizo”.
‘Badala
ya kucheza mpira, mchezaji anaingilia masuala ya usajili na kutaka
kusajiliwa kwa rafiki zake…kiukweli inachanganya na kuwa ajabu”
‘Alifanya kila kitu akiwa Anzhi, isipokuwa kucheza mpira.’
Ujio
mpya: Eto’o alijunga na Chelsea kwa uhamisho wa bure katika majira ya
kiangazi mwaka huu baada ya klabu ya Anzhi kuamua kuwauza wachezaji
wake ghali
Akirejea
uhusiano wao uliovunjika baadaye, Carlos aliongeza: ‘Nilijiunga na
klabu na kwa mara yangu ya kwanza tulimaliza ligi tukiwa tano bora”.
‘Tuliweza
kuiweka klabu katika soka la kisasa na kitaalamu. Mwaka wa pili
tulimsajili Eto’o na niliitawala timu na kuwaunganisha wachezaji na
kufanya kazi vizuri na kocha. Niliiweka Anzhi kuwa miongoni mwa timu
bora”.
Umeonya : Jose Mourinho anaweza kumuweka Eto’o katika mstari wa mafanikio
0 comments:
Post a Comment