Thursday, September 5, 2013


Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
BINGWA wa kukata upepo katika riadha, Usain Bolt amewataka mashabiki wa Manchester United kuwa nyuma ya  Marouane Fellaini na kumuunga mkono kwa hali ya juu mara tu atakavaa jezi nyekundu ya Old Trafford.
Nyota huyo anayeshikilia rekodi ya dunia  katika mbio za mita 100 na 200 ,  na shabiki mkubwa wa United alisema hayo huku akishikilia jezi ya timu ya taifa ya Ubelgiji yenye jina la Fellaini mgongoni.
Hii imekuja muda mfupi tu tangu Bolt amtake kocha wa Man United, David Moyes kusajili kabla ya dirisha la usajili la majira ya kiangazi kufungwa.
Huge United fan: Usain Bolt showed off a Belgium shirt with Marouane Fellaini on the backShabiki wa kufa wa United: Usain Bolt akionesha jezi ya timu ya taifa ya Ubelgiji yenye jina la Marouane Fellaini mgongoni
“David Moyes, tunahitaji kiungo mjuzi, ambaye anaweza kupiga pasi na kutengeneza nafasi, mwenye uwezo mkubwa kumiliki mpira na mtu thabiti, tunataka muda huu”. Alisema Bolt akimuambia kocha wa Man United.
Lakini baaada ya Fellaini kusajiliwa, labda Bolt ametulizwa moyo kwa ushabiki wake wa soka.
Pia aliongea kitu ambacho hakikutarajiwa na wengi kuwa atastaafu riadha baada ya mashindano ya Olympiki ya mwaka 2016 huko Rio.
‘Nadhani nimejijenga jina na nataka kwenda kushiriki mashindano hayo na kufanya vizuri, nadhani itakuwa wakati muafaka wa kusataafu nikiwa juu na kutawala kwa muda mrefu”. Alisema Bolt.
Ready to go: Bolt admitted that he may not have any motivation after the Rio OlympicsTayari kustaafu: Bolt amesema hataendelea tena na riadha baada Olympic za Rio

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video