Na Meg Muigai, Lindi
Leo
tunashuhudia uzinduzi wa kampeni ya usalama barabarani unaofadhiliwa na
BG Tanzania katika mkoa wa Lindi, kusini mwa Tanzania. Baada ya
kupewa kazi ya kufanya utafiti kuhusu ajali za barabarani na Chuo cha
Taifa cha Usafirishaji (NIT), kampuni ya gesi ilibaini fursa za
kushirikiana katika kuimarisha maadili ya usalama barabarani miongoni
mwa wakazi wa Lindi .
Chuo
cha Taifa cha Usafirishaji kilibaini visababishi vinne vya mara kwa mara
vya ajali za barabani mkoani Lindi ambavyo ni:waendesha pikipiki
wasiozingatia maadili ya uendeshaji; mwendo kasi wa waendesha
pikipiki;kuendesha huku umelewa; na ukosefu wa alama au ishara za
barabarani. BG Tanzania
imeazimia kupunguza kiwango cha ajali kwa kufadhili utoaji wa mafunzo ya
usalama barabarani.Hii inaenda sambamba na juhudi za mkoa katika
kupunguza ajali za barabarani.
Mkuu
wa masuala ya Sera na Ushirika wa kampuni ya BG Tanzania, Fred Kiboya,
alihudhuria kwenye sherehe na alisema “Hili ni tukio muhimu kwa BG
Tanzania. Kama kampuni tunaamini katika usalama, na tunataka
kuhakikisha kuwa, uwepo wetu kusini mwa Tanzania unajenga jamii salama
na zenye mafanikio zaidi.Tunaendesha programu ya aina hii Mtwara Mjini,
ambapo waendesha pikipiki 600 wanapatiwa mafunzo, na sasa tunarudia
zoezi mkoani Lindi.”
Mkoani
Lindi, waendesha pikipiki mia mbili watanufaika katika awamu ya kwanza
ya programu hii. Kila mmoja atapewa mafunzo ya zaidi ya siku kumi ambapo
siku sita zitakuwa kwa ajili ya mafunzo ya nadharia na siku nne
zitakuwa kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo. Hii itajumuisha utambuzi wa
alama na ishara za barabarani, nadharia za uendeshaji wa
kujihami,uendeshaji unaofaa, mkao sahihi katika uendeshaji na udhibiti.
Baada ya kumaliza mafunzo kwa ukamilifu, washiriki watapewa cheti cha
umahiri katika uelewa wa usalama barabarani pamoja na leseni ya
uendeshaji. Kundi la washiriki limechukuliwa kutoka katika kata za
mchinga, Kitomanga, Rutamba, Nyangao na Milola.
Gharama
za mafunzo ni Sh. 220,000/-kwa kila mshiriki,hii ikimaanisha kwamba
,kwa ujumla, BG Tanzania imewekeza Shilingi 44,000,000/- kwa ajili ya
mafunzo na upatikanaji wa leseni katika awamu hii. Awamu ya pili,ambayo
itajumuisha waendesha pikipiki wengine 200 itapangwa baadaye.
Mgeni
rasmi kwenye tukio alikuwa Mheshimiwa Saidi Mtanda, Mbunge wa Jimbo la
Mchinga ;ambapo Mhandisi Dk. Ezekial Mganilwa, Mkuu wa Chuo cha Taifa
cha Usafirishaji aliiwakilisha taasisi yake. Bwana Machumu Leonard,
Afisa wa Usalama Barabarani wa Mkoa wa Lindi alihudhuria akiiwakilisha
Ofisi ya Kamishina wa Polisi wa Mkoa pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa
ACP Mwakanjiga
0 comments:
Post a Comment