Katibu mkuu wa BFT, Makore Mashaga |
SHIRIKISHO LA NGUMI TANZANIA
Taarifa kwa vyombo vya habari.
Yah:- BFT kutotambua viongozi waliojivika uongozi wa kuongoza Chama cha
ngumi Mkoa wa Dar es alaam (DABA) 21 SEPT. 2013.
Shirikisho
la ngumi Tanzania (BFT) halitambui uongozi uliojiingiza madarakani wa
kuongoza chama cha ngumi mkoa wa Dar es salaam ( DABA ) kiujanja ujanja
bila kuzingatia Sheria na Kanuni za Baraza la Michezo Tanzania (BMT) ,
katiba ya Chama cha ngumi cha dunia (AIBA), Shirikisho la ngumi
Tanzania (BFT) na katiba ya Chama cha Ngumi mkoa wa Dar es salaam
(DABA).
Uongozi
huo ulijingiza madarakani tarehe 21/09/2013 katika ukumbi wa DDC
Mlimani bila ya kuwa na kibali cha kutoka BFT wala Kibali kutoka Ofisi
ya afisa michezo wa mkoa wa Dar es salaam, ambao wao kiutaratibu ndio
walikuwa na mamlaka ya kutoa kibali cha Kufanyika kwa uchaguzi huo na
kuusimamia kwa mujibiu wa sheria zinazoongoza michezo hapa Tanzania.
Badala
yake genge la watu wachache walijikusanya na kupeana fomu kinyume na
taratibu kwa kujuana na hatimaye kupeana taarifa wakakutana na kujivika
madaraka kwa nyadhifa mbalimbali bila kufata taratibu.
BFT
haikubaliani na jambo hilo kwa kuwa kati ya waratibu wa zoezi hilo
waliojivika uongozi wa juu ni wale waliokuwa katika uongozi wa
shirikisho la ngumi Tanzania BFT na kupelekea Tanzania kufungiwa
uanachama na chama cha ngumi cha dunia (AIBA) kwa miaka miwili na zaidi
kusababisha bondia aliyekuwa tegemeo na Taifa Petro Mtagwa kufungwa
jela miaka 15 nchini Mauritius pia kusababisha bondia Emillian Patrick
kushindwa kushiriki Mashindano ya Olimpiki 2008 baada ya kuwa amefuzu
kwa tuhuma za kula njama za kusafirisha madawa ya kulevya.
Kibaya
zaidi wengi waliopewa madaraka hawakuja fomu za kuomba nafasi kama
walivyopewa na hawakuwepo katika uchaguzi huo, wala hawakufanya usaili
kama taratibu zilivyo.
Wanachama
halali waliokuwa wanatakiwa kuwepo katika uchaguzi huo mfano viongozi
wa chama cha ngumi Temeke hawakupewa taarifa za uchaguzi na wameleta
malalamiko ofisi za BFT.
Uchaguzi
huo umekiuka katiba kwa kuhusisha mabondia na viongozi wa ngumi za
kulipwa kitu ambacho ni tofauti na katiba zote za ngumi za ridhaa.
BFT
itachukua hatua kali za kimaadili na kinidhamu kwa wote waliohusika na
zoezi hilo na kusisitiza kwa wanachama wote kuzingatia sheria za
uchaguzi wanapofanya uchaguzi wa vyama vyao na kuwataka wengine
kutokujiingiza kwa magenge ambayo historia inaonyesha wamekuwa wasubufu
wa mambo mbalimbali tokea uongozi wa Narcis Tarimo enzi za TABA kwa
masilahi yao binafsi.
Zaidi
tutashirikiana na Ofisi ya Afisa michezo wa Mkoa kuhakikisha uchaguzi
unafanyika wa kupata viongozi kwa kuzingatia taratibu.
Taarifa hizi zinaletwa kwenu na
Makore Mashaga
Katibu Mkuu.
0 comments:
Post a Comment