Sunday, September 1, 2013

1. Seif akifunguaMakamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akifungua Mkutano maalum wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) leo, katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui mjini Zanzibar. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Zanzibar), Shaka Abdul Shaka, Katibu  Mkuu wa UVCCM aliyemaliza muda wake, Martine Shigela na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamis na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mboni Mhita, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana. (Picha na Bashir Nkoromo).
2. Sadifa Juma akifunguaMwenyekiti wa UVCCM, Taifa, Sadifa Juma Hamis akimkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano huo
3. Seif na Kinana wakiongoza kumuombea KarumeMakamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Ali Seif Iddi akiongoza dua kwenye kaburi la Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Abeid Amani Karume, Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui, Zanzibar Kabla ya kufungua Mkutano maalum wa Baraza Kuu la UVCCM, leo. Wengine ni kutoka kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Bara)  Mfaume Ally Kizigo, Makamu Mwenyekiti wa UVCCM, Mboni Mhita na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamis na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Zanzibar), Katibu Mkuu wa UVCCM Mstaafu, Martine shigela na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana. (Picha na Bashir Nkoromo)
4. shigela akimkaribisha SadifaKatibu Mkuu wa CCM Mstaafu, Martine Shigela akitoa shukrani baada ya kumaliza muda wake, kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la UVCCM Kisiwandui Zanzibar na nafasi yake kuchukuliwa na Katibu Mkuu mpya Situs Mapunda.
5. Nape, Makamba na Nchimbi wakitetaWaalikwa kwenye kikao cha Baraza kuu la UVCCM, lilifanyika leo Kisiwandui, Zanzibar, Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi Nape Nnauye akishauriana jambo na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba na Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimi kwenye kikao hicho. (Picha na Bashir Nkoromo).
6. Wajumbe ukumbini (1)Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho cha Baraza Kuu la UVCCM, mjini Zanzibar leo.
7. Balozi seif akimsalimia KinanaMakamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Ali Seif Iddi akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Adulrahman Kinana baada ya kuwasili Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui Zanzibar kufungua kikao cha Baraza Kuu la UVCCM.
8. Vuai, akishauriana jambo na Kinana, ShigelaKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (Katikati) akiwasikiliza, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai na Katibu Mkuu Mstaafu wa UVCCM, Martin Shigela, nje ya Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui mjini Zanzibar kabla ya kikao cha Baraza Kuu kuanza, leo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video