Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MAKAMU
bingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Azam fc inajiandaa
kuvuna pointi tatu muhimu katika mchezo wa kesho dhidi ya Ashanti United
, `Watoto wa jiji` , uwanja wa Azam Complex baada ya kupata sare ya
kufungana bao 1-1 na Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera
jumamosi ya wiki iliyopita.
Afisa
habari wa klabu hiyo, Jafar Idd Maganga amesema kocha mkuu wa klabu
hiyo Sterwart John Hall ameshabaini makosa yaliyomnyima ushindi katika
mchezo uliopita, hivyo anaendelea kuyafanyia kazi kabla ya kibarua cha
kesho.
“Hatujaanza
vizuri ligi msimu huu, tumetoa sare mbili na kushinda mechi moja, si
matokeo mazuri kwetu, lakini mpira wa miguu ni mchezo wa makosa, kikubwa
tuko tayari kwa mechi ijayo na watoto wa jiji, Ashanti United, Kocha
wetu anafanyia kazi makosa ya vijana wake”. Alisema Jafar.
Jafar
alisema baada ya kubanwa na Kagera Sugar, wamegundua kuwa ligi ya mwaka
huu ina ushindani mkubwa na hata ukiangalia wanaoongoza kileleni nje
ya timu nne za juu msimu uliopita.
“Azam
fc ni klabu iliyofanya maandalizi mazuri, tunahitaji kushinda mechi
ijayo ili kuendelea kujipanga kuingia rasmi katika ushindani wa kuwania
taji msimu huu”. Alisema Jafar.
Afisa
habari huyo aliongeza kuwa nia ya Azam siku zote ni kuleta mapinduzi ya
soka, hivyo wanaendeleza mipango hiyo kwa kuhakikisha kikosi chao
kinakuwa bora muda wote kutokana na kusheheni makocha wazuri na
wachezaji wenye uwezo na morali kubwa.
Kwa
sasa Azam fc wapo nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na
pointi tano kibindoni, ambapo mchezo wa kwanza walitoka sare ya 1-1 na
Mtibwa Sugar uwanja wa Munungu, mchezo wa pili walishinda mabao 2-0
dhidi ya Rhino Rangers mjini Tabora na mechi ya tatu wakatoka sare ya
bao 1-1 na Kagera Sugar juzi mjini Bukoba mkoani Kagera.
Msimu
uliopita Azam fc walitwaa nafasi ya pili na kuliwakilisha taifa katika
michuano ya kombe la shirikisho na kufika hadi Raundi ya tatu na
hatimaye kutolewa kwa mbinde na AS FAR Rabat ya Morocco.
0 comments:
Post a Comment