Wednesday, September 4, 2013

DSC_5798Ashanti United “Watoto wa jiji” walianza ligi kuu soka Tanzaniabara kwa kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa mabingwa  Yanga uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, na mechi ya pili wakapigwa 1-0 na Mgambo Jkt Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga
……………………..
Na Baraka Mpenja , Mbeya
KLABU ya Ashanti United  imewaomba mashabiki wake kutokata tamaa na matokeo ya mechi za kwanza za ligi kuu soka Tanzania bara ambapo walifungwa 5-1 na Yanga na kufungwa 1-0 na Mgambo JKT,  kwani chanzo cha kufungwa ni ugeni wa wachezaji wake katika mikikimikiki hiyo.
Akizungumza na Mtandao wa MATUKIO DUNIANI, Kocha mkuu wa klabu hiyo, Hassani Banyai amesema kadri siku zinavyozidi kwenda kuna mabadiliko makubwa sana katika kikosi chake na kufikia mchezo wa septembe 14 dhidi ya JKT Ruvu atakuwa amefanya mabadiliko makubwa kwa wanandinga wake.
“Unajua mechi ya kwanza tulipocheza na Yanga tulifungwa kwasababu sisi tunatumia vijana ambao hawana uzoefu na nadhani tulizidiwa na wenzetu kutokana na uzoefu wao, lakini mechi ya pili dhidi ya Mgambo JKT vijana walicheza vizuri na kwa sasa vijana wanaimarika na watafanya makubwa:” Alisema Banyai.
Banyai  ameongeza kuwa kupata matokeo mabaya mechi mbili sio tatizo kwani mpaka sasa wamebakiwa na mechi 24 kati ya 26 za msimu mzima, hivyo wana nafasi ya kujipanga ili wapate matokeo mazuri.
“Kikubwa niwaombe wachezaji wa Ashanti , watambue wajibu wao, hivyo lazima wajitume na wafikirie kuisadia timu kwanza,  watambue kuwa kujituma ndio siri ya mafanikio, pia  ugali wao uko hapo”. Alisisitiza Banyai.
Kocha huyo amewaasa mashabiki na wanachama wao kuwa wavumilivu na kupoteza mechi isiwe tabu kwao kwani safari bado ni ndefu sana, kinachotakiwa ni kuwa na umoja na mshikamano zaidi.
Akizungumzia mchezo ujao dhidi ya JKT Ruvu, Banyai amekiri kuwa mechi hiyo ni ngumu na watakabiliana na kocha Mbwana Makata ambaye ana uzoefu mkubwa na ligi kuu, pia timu yake iko pamoja kwa muda mrefu, ila wanaendelea kujipanga vizuri kuhakikisha wanafanya vizuri.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video