Na Buberwa Jackob
Kwanini
Vibali vyote vya kuishi wageni visifutwe na kusajiliwa upya?. Msako
lazima uwe na kasi kubwa tena uanzie mji mikubwa kama Dar, Arusha…
Kuanzia
mwezi julai 2013 kiongozi mkuu wa nchi yetu rais Dk.Jakaya Kikwete
katoa agizo kuwa raia wote wa kigeni ambao ni wahamiaji haramu wamepewa
siku 14, kuondoka au kujisalimisha katika vyombo vya dola.
Agizo
hili la rais lina lengo zuri tu kwa watanzania na usalama wa
watanzania, lakini utekelezwaji wake umekuwa hauna kasi, kwani idadi ya
wahamiaji haramu walio jisalimisha ni ndogo kulingana na waliopo nchini,
na kati ya hao waliojisalimisha ni wahamiaji waliopo nje ya miji mkubwa
sio katika miji mikubwa kama Dar ,Arusha nakwingineko !
Cha
kushangaza kwamba kuna baadhi ya wahamiaji haramu au halali wanakiuka
kwa namna moja au nyingine sababu zinazowafanya kuwepo nchini Tanzania.
mfano raia wa kigeni aliyekuja nchini kwa kufanya kazi fulani na akapewa
kibali kwa ajili hiyo anakiuka kwa taratibu za uhamiaji na kuanza kuwa
mfanyi biashara ya baa au dangulo fulani! au pengine kujiingiza katika
biashara ambayo mzawa anaweza kuifanya, na huku vyombo vya usalama
vikimwangalia !
Hivi kuna uhalali wa kisheria Raia wa kigeni asiye na hata asili ya Tanzania kumiliki nyumba au Ardhi ?
Watanzania
wengi wamekuwa wakilalamika juu ya ongezeko la raia wa kigeni hususan
raia wa nchi za ulaya, Asia na nchi za kiarabu kumiliki au kununua
nyumba na ardhi nchini , mfano wachina wanamiliki majumba au ardhi,
huenda wakawa wanakiuka sheria fulani za nchi,na watanzania wanao
wauzia nyumba wageni hao nao pia wanajisaliti au kuisaliti nchi.
Ukiwikaji
wa sheria za ajira ! mchina anapofanya kazi ya kuuza duka na mitumba au
kubeba zege ! Mzungu anapokuja kutalii na baadaye kupata ajira ya
muhudumu wa hotel ! hili nalo neno?
Bendi za muziki zinapo ajiri wanenguaji kutoka nje ya nchi!
Ndio
maana watanzania walio wengi wanaona kuwa ipo haja kwa serikali
kuvifuta vibali vyote vya wageni na kuanza zoezi la kuvitoa upya na
kuvihakiki kwa kupitia Wizara ya mambo ya ndani.
Kama
Rais JK kashatoa agizo tangu mwezi julai mbona utekelezaji wake una
mwendo wa pole ? wakati kiongozi mkuu wa nchi, ambaye ndiye amiri jeshi
mkuu kishaagiza siku 14 tu kila muhamiaji haramu aondoke sasa kwanini
msako usianze katika kutekeleza agizo la mkuu wa nchi?.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Rais JK
0 comments:
Post a Comment