Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Tanzania Bw. Phillipe Corsaletti (wa
pili Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Amend Tanzania Bi.
Kate Raum ( wa pili Kulia) wakikata utepe kukabidhi rasmi miundo mbinu
ya usalama barabarani kwa Mwakilishi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya
Kinondoni Jijini Dar es Salaam Bw. Faustine Kikove mbele ya Walimu wakuu
wa Shule za Msingi za Bryceson, Bi. Apolonia Kiwango (kushoto) na Shule
ya Msingi Mburahati, Bw. Mahamudu zilizopo kata ya Mburahati. . Sherehe
za makabidhiano ya vifaa hivyo ni ya sehemu maadhimisho ya wiki ya
nenda kwa usalama barabarani Jijini Dar es Salaam zilizoanza Jumatatu
Septemba 23, 2013. Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Tanzania Bw. Phillipe CorsalettI
(wa pili kushoto) pamoja na Walimu Wakuu wa shule za Bryceson na
Mburahati Jijini Dar es Salaam, Bi. Bi. Apolonia Kiwango (kushoto) na
Bw. Mahamudu (kulia) wakitizama moja ya alama za michoro zilizobuniwa na
Kampuni za Amend Tanzania na Puma Energy inayofundisha wanafunzi hatua
muhimu za kufanya kabla ya kuvuka barabara. Sherehe za uzinduzi huo
ulifanyika jumanne Septemba 24, 2013 zikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
wiki ya nenda kwa usalama Barababarani Jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi
wa Shule za msingi za Bryceson na Mburahati zilizopo katika Halmashauri
ya Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam wakionesha mabegi yenye
ujumbe unaosomeka “kuwa salama barabarani” waliyokabidhiwa jumanne
Septemba 24, 2013 kutoka kutoka kwa PUMA Energy ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama Barabarani Jijini Dar es
Salaam.
Wanafunzi
wa shule za msingi za Bryceson na Mburahati zilizopo katika Halmashauri
ya Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam wakiimba kwa vitendo wimbo
wa usalama barabarani wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya
PUMA Energy Tanzania Bw. Phillipe Corsaletti (wa pili Kushoto) wakati wa
maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani Jijini Dar es
Salaam
0 comments:
Post a Comment