Dr.
Bamuhimbisa Richard kutoka AAR Healthcare akitoa mafunzo kwa washiriki
wa BSS 2013 ya jinsi ya kuishi maisha bora kwa kuwa waangalifu na afya
zao,walipokua kwenye kambi yao Mbezi Beach Washiriki wa Bongo Star Search wakipata vipimo vya BMI na BP kabla ya kupanda jukwaani
Muuguzi Salome Mkilima kutoka AAR akimpima BP mshiriki wa BSS 2013 kambini Mbezi Beach Dar-es-salaam
Daktari Richard kutoka AAR akitoa kipimo cha BMI kwa mmoja ya washiriki wa BSS 2013 kambini mbezi Dar-es-salaam Mshiriki
wa BSS Elizabeth Mwakijambile akiongea na waandishi wa habari baada ya
kupata vipimo vya afya kutoka AAR walipoenda kutembelewa kambini kwao
Mbezi.
Afisa
Mahusiano wa AAR HealthCare Amisa Juma akiwapa mafunzo washiriki wa BSS
2013 kuhusu afya zao ,kuchoto ni Bi, Fatma Omary, Maina Thadei na Amina
Chibaba
AAR Healthcare wakiwa na washiriki wa BSS 2013
………….
Hivi
karibuni AAR Healthcare imefanya vipimo vya afya kwa washiriki wa
Bongo Star Search mwaka 2013, vipimo hivyo vikiwamo BMI, BP pamoja na
kipimo cha kisukari
Washiriki
hao ambao kwa sasa wamebaki 15 ,walipewa pia mafunzo ya kiafya
kutoka kwa Madactari wa AAR ya jinsi ya kuishi maisha yao kwa afya
njema.
“Dhumuni
la kuwafanyia washiriki vipimo vya afya, ni wao wenyewe kuweza
kutambua afya zao kabla ya kuanza kupanda jukwaani, kupata ushauri
wa jinsi ya kutunza afya zao kwa kipindi chote cha mashindano na hata
baada ya mashindano” . Alisema Afisa Mahusiano wa AAR Amisa Juma.
Bi.
Juma alimalizia kwa kusema “ Sisi kama wadau wakubwa katika afya
nchini, tumegundua vijana ndo waathirika wakubwa wa afya, kwaiyo
tumeamua kutumia jukwaa hili la BSS kuweza kusaidia na kutoa mchango
mkubwa kwa washiriki na jamii kwa ujumla” .
Hii ni mara ya pili kwa AAR kudhamini mashindano haya ya BSS, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2011.
0 comments:
Post a Comment