Serikali
ya Kenya kupitia kwa waziri wake wa usalama Joseph Ole Lenku imesema
kuwa watu 59 wamefariki katika shambulizi la kigaidi lililofanywa na
wanamgambo wa Al Shabaab na wengine 175 kujeruhiwa.
Waziri
Ole Lenku amesema kuwa idadi ya magaidi walio ndani ya jengo hilo ni
kati ya kumi na kumi na tano na haijulikani ikiwa wanwazulia waathiriwa
au waathiriwa wamjificha katika sehemu mbali mbali z jumba la Westgate.
Shirika
la Red Cross awali katika taarifa yake ilisema kuwa watu 43 ndio
waliofariki na zaidi ya 50 kujeruhiwa huku wengine wakitekwa nyara
katika mashambulizi la kigaidi Jumamosi mchana.
Milio
ya risasi imeweza kusikika katika jengo la Westgate mjini Nairobi
Kenya, ambako wanamgambo wa Al shabaab wanawazuilia mateka ambao idadi
yao haijajulikana hadi sasa.
Wanajeshi
wawili walijeruhiwa katika ufyatulianaji huo na kukimbizwa hospitalini
kwa matibabu huku watu wawili wakinusuriwa asubuhi ya leo.
Hadi
sasa jeshi limeweza kudhibiti hali nje na ndani ya jengo hilo, magari ya
kijeshi yakiwa yameletwa katika eneo hilo huku polisi na wanajeshi
wakijaraibu kuwanusuru baadhi ambao wangali wanazuiliwa ndani ya jengo
hilo.
Watu
39 wameuawa baada ya wanamgambo hao kushambulia jengo hilo mwanzo katika
eneo la kuegeshea magari na kisha kuingia ndani ya mikahawa na maduka
katika jengo hilo lenye ghorofa nne na kuwpaiga watu risasi kuholela.
Kuna taarifa kuwa wanamgambo hao wako ndani ya duka moja kubwa katika jengo hilo.
Rais
Kenyatta anasema kuwa baadhi ya waliofariki ni jamaa zake. Miongoni mwa
waliofariki pia ni mwanadiplomasia wa Canada na raia wawili wa Ufaransa.
Rais Kenyatta anasema kuwa wale waliohusika lazima wakabiliwe na mkono
wa sheria.
Jamaa
na marafiki waliofika kujua hali ya jamaa zao wamezuiwa kuingia ndani
ya jengo hilo. Wengi wa waathiriwa walifariki kutokana na majeraha yao.
KUTOKA BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment