Gladness Mushi, Arusha.
ZAIDI ya wakulima mia moja kutoka zaidi ya vijiji vitano wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wamenufaika na mpango wa elimu ya matumizi bora ya mbegu za kilimo ambazo zina uwezo mkubwa wa kustahimili ukame hususan kipindi hiki mbacho nchi inakabiliwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.
ZAIDI ya wakulima mia moja kutoka zaidi ya vijiji vitano wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wamenufaika na mpango wa elimu ya matumizi bora ya mbegu za kilimo ambazo zina uwezo mkubwa wa kustahimili ukame hususan kipindi hiki mbacho nchi inakabiliwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Ambapo wakulima hao wamepata elimu hiyo kutoka kampuni ya Northen Seeds Company Ltd iliyopo mjini moshi inayozalisha mbegu bora za kilimo kwa ajili ya kusaidia wakulima kuweza kupata mazao ya kutosha kutokana na kutumia mbegu hizo ambazo zinastahimili ukame.
Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa kampuni hiyo, Magreth Alson Shangali wakati akizungumza katika maonyesho ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro vilivyopo jijini hapa.
Alisema kuwa , kampuni hiyo imekuwa ikizalisha mbegu za mahindi, alizeti, mtama, mbegu za mboga mboga, nyanya, mchicha , mnafu, bamia na gongwe ambapo mbegu hizo zimekuwa zikiwafikia wakulima kwa bei nafuu ambayo inamwezesha pia mkulima wa chini kumudu gharama hizo.
Magreth aliongeza kuwa, kampuni imefanikiwa kutoa elimu kwa wakulima wa vijiji hivyo jinsi ya matumizi ya mbegu hizo ambazo zinastahimili ukame ,na kuweza kuzalisha chakula cha kutosha hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inakabiliwa na ukame mkubwa.
Alifafanua zaidi kuwa, baada ya wakulima hao kupatiwa elimu hiyo wameweza kuwa kiasi kikubwa kulima kilimo chenye tija na kupata mazao ya kutosha kutokana na mbegu hizo kukomaa kwa kipindi cha muda mfupi .
‘sisi pamoja na kuwa ni wazalishaji wa mbegu mbalimbali za kilimo lakini huwa tunatoa elimu hiyo kwa wakulima wetu kila baada ya miezi sita na mbegu zetu tumekuwa tukisambaza nje ya mkoa wa Kilimanjaro pia kutokana na ubora mzuri uliopo katika mbegu hizo hususani kustahimili ukame na kukomaa kwa kipindi cha muda mfupi tofauti na mbegu nyingine ‘alisema Magreth.
0 comments:
Post a Comment