Na Baraka Mpenja
Hatimaye mechi ya Ngao ya jamii kuashiria kufungiliwa kwa pazia la ligi kuu soka Tanzania bara baina ya mabingwa watetezi klabu ya Yanga dhidi ya makamu bingwa, Azam fc zote za jijini Dar es salaam katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam zimemalizika kwa wanajangwani kuwafumua wapinzani wao bao 1-0 lililofungwa na Salum Telela katika dakika ya 2 ya mchezo huo akiunganisha krosi safi ya Didier Kavumbagu.
Mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi wa kati Oden Mbaga, akisaidiwa na Hamisi Chang’walu na Omar Kambangwa wote wa Dar es Salaam, hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zikimalizika, Yanga walikuwa kifua mbele kwa walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Nao Azam walipata nafasi kadhaa za kufunga, lakini washambuliaji wao wakiongozwa na John Bocco “Adebayor” walishindwa kubadili nafasi hizo kuwa magoli.
Kabla ya mechi hiyo tambo zilitawala kwa mashabiki wa tmu hizo, huku mashabiki wa Simba wakiishangila Azam kwa nguvu zote, lakini mashabiki wa Yanga walionekana kuwa na matumaini ya ushindi kwani walifika kwa wingi sana uwanjani na mwisho wa mchezo huo wametoka na vicheko.
Azam fc walikuwa Afrika kusini kujiandaa na mechi za ligi kuu Tanzania bara pamoja na huu wa leo ambao wamepoteza kwa kipigo hicho cha bao la mapema la Telela aliyecheza vizuri zaidi katika mchezo wa leo na kama angekuwa makini basi angeifungia timu yake mabao zaidi.

Azam FC; Aishi Manula, Erasto Nyoni/Joackins Atudo dk46, Waziri Salum, David Mwantika, Aggrey Morris, Himid Mao, Kipre Tchetche, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’/Gaudence Mwaikimba dk74, Kipre Balou/Ibrahim Mwaipopo dk62 na Khamis Mcha.
PICHA KWA HISANI YA MTANDAO
0 comments:
Post a Comment