Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Dar Young Africnas wametamba kuwabamiza wapinzania wao Azam fc “wana lambalamba” katika mchezo wa ngao ya hisani agosti 17 mwaka huu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kuashiria kufunguliwa pazia la ligi kuu msimu wa 2013/2014.
Akizungumza na Mtandao wa FULLSHANGWE, Afisa habari wa Yanga, Baraka Kizuguto amesema kikosi chao kinaendelea vizuri na mazoezi kujiandaa na mchezo huo muhimu kwao na wanajiandaa kushinda kutokana na klabu hiyo kusheheni wachezaji nyota wenye kiwango cha juu.
“Yanga ina kikosi kizuri mno kwa sasa, hatuna wasiwasi kabisa, sisi tunaendelea na mazoezi ya kujiandaa kuwakabili wapinzani wetu katika mchezo huo wa Ngao ya jamii”. Alisema Kizuguto.

“Azam fc ni wazuri, itakuwa mechi nzuri sana, lakini sisi Yanga tunajiandaa kama kawaida yetu kutoa dozi, lazima tuwafunge wapinzani wetu na kutwaa kombe la ngao ya hisani ili kuendelea kuwajenga wachezaji kisaikolojia pamoja na mashabiki wetu kuelekea kutetea ubingwa wetu wa ligi kuu soka Tanzania bara”. Alisema Kizuguto.

Said alisema walianza kwa kufungwa mabao 3-0 na Kaizer Chief inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika kusini, lakini kwa kiasi kikubwa walipata kile walichokuwa wanakihitaji, na leo hii watacheza mechi ya pili dhidi ya Mamelodi Sundwons .
Meneja huyo alisema watarejea nchini Agosti 13 kufanya maandalizi ya mwisho kujiandaa na mchezo wa ngao ya Hisani ambapo amesema watafanya vizuri na kuwafunga Yanga kutokana na maandalizi mazuri wayapatayo nchini Afrika kusini.
0 comments:
Post a Comment