Thursday, August 8, 2013

Na Baraka Mpenja 
Mabingwa wa soka Tanzania bara, klabu ya Yanga ya Dar es salaam wameendelea kutamba katika mechi za kirafiki kuelekea msimu mpya wa ligi kuu unaotarajia kuanza kushika kasi agosti 24 mwaka huu,baada ya leo kuitungua 3Pillars FC ya Nigeria bao 1-0 uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam.
Katika mchezo wa leo, mshambuliaji mpya wa Yanga SC, aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro majira haya ya kiangazi, Hussein Javu ameifungia klabu yake bao la pekee katika ushindi wa leo.
Hilo linakuwa bao la pili kwa Javu tangu ajiunge na Yanga akifunga katika mechi mbili mfululizo.
3PILLARSNAYANGA6Mashine mpya ya kufumania mabao jangwani, Hussein Javu akiwaonesha kazi wachezaji wa 3Pillars
Mchezo uliopita dhidi ya klabu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar ambao Yanga walishinda mabao 3-1, Javu alitia kambani bao akitokea benchi.
Afisa habari wa klabu ya Yanga, Baraka Kizuguto amesema Katika mchezo wa leo, mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara Young Africans waliingia uwanjani kwa lengo la kusaka ushindi katika michezo ya kirafiki ya kujipima ubavu kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu soka ya Vodacom  Tanzania bara msimu wa 2013/2014.
3PILLARSNAYANGA7Jerry Tegete akionesha ufundi wake katika mechezo wa leo
Hata hivyo Baraka aliongeza kuwa wanajangwani wakiongozwa na washambuliaji wake wapya, Hussein Javu na Mrisho Ngassa “Anko”  waliojiunga na kikosi msimu huu, walikosa nafasi za wazi, lakini Kocha wao Ernie Brandts atafanyia kazi tatizo hilo.
Kesho kikosi cha Yanga hakitakua na mazoezi na wachezaji wote watakua na mapumziko kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid na waterejea tena mazoezini siku ya jumamosi asubuhi katika uwanja wa Loyola kuendelea kujifua na maandalizi ya Ligi Kuu.
(PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL)

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video