Sunday, August 11, 2013

YANGAVSVILLA6 (1)Mshambuliaji wa wa Yanga, Jerry Tegete akifanya mambo yake katika mchezo wa leo
YANGAVSVILLA7Mchezaji bora wa ligi kuu msimu uliopita, beki wa kati wa klabu ya Yanga, Kelvin Yondan akiwakomalia wachezaji wa Villa
(Picha na Richard Bukos/GPL)
Na Baraka Mpenja 
Mabingwa wa soka Tanzania bara, klabu ya Dar Young Africans leo wameshuka dimbani katika mchezo wa kirafiki kuwakabili wanaume kutoka Uganda klabu ya  Sports Club Villa.
Mchezo huo wa kukata na shoka umepigwa katika dimba la taifa na kushuhudia dakika 90 zikimalizika  kwa matokeo ya ya Yanga kuwabamiza Villa mabao 4-1.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Mrisho Ngasa dakika 7, Nadir Haroub Canavaro dakika 27 , Didier Kavumbagu dakika ya 30 na Haruna  Hakizimana Fadhil NIYONZIMA dakika ya 62.
Afisa habari wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema mechi ya leo ilikuwa nzuri sana na kipimo kizuri kwao ingawa kipindi cha pili waliwazidi sana wapinzani wao.
“Villa walicheza vizuri kipindi cha kwanza, lakini sisi tulitulia zaidi na kuwazidi maarifa na kutumia nafasi tulizopata na hivyo kuendeleza wimbi la ushindi katika mechi za majaribio kabla ya kuanza ligi kuu Agosti 24 mwaka huu”. Alisema Baraka.
Kizuguto alisema mechi ya leo ni muendelezo wa maandalizi yao kuelekea mchezo wa kukata utepe wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Azam fc waliopo nchini Afrika kusini kujiweka sawa.
Majogoo wa kampala waliingi uwanjani wakiwa na kumbukumbuya kupigwa mabao 4-1 hapo jana na wekundu wa msimbazi Simba.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video