Thursday, August 8, 2013

Na Baraka Mpenja 
MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Yanga ya Dar es salaam, leo inatarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya 3Pillars Football Club ya Nigeria uwanja wa Taifa ikiwa ni maandalizi ya kipute cha Ngao ya Hisani dhidi ya Azam FC pamoja na ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2013/2014 inayotarajia kuanza kushika kasi Agosti 24 mwaka huu.
Afisa habari wa klabu ya Yanga, Baraka Kizuguto amesema maandalizi kwa ajili ya mechi hiyo yanakwenda vizuri na leo hii vijana wa jangwani wamejipanga kuonesha mpira wa hali ya juu.
“Hii ni mechi ya kujiandaa na mechi dhidi ya Azam fc agosti 17 mwaka huu ambao wapo Afrika kusini, itakuwa mechi nzuri sana kwani mpaka sasa hatuna majeruhi yeyote, wachezaji wana morali kubwa, hivyo mashabiki wa Yanga, klabu ya wananchi wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa leo hii”. Alisema Kizuguto.
e76dYanga1Kosi la Kwalalumpa Malysia, Dar Young Africans, lililojaa maarifa ya mzungu Ernie Brandts
Kizuguto alitaja kiingilio cha juu katika mechi hiyo kuwa ni shilingi elfu 15 na kiingilio cha chini kuwa ni shilingi elfu tano hivyo mashabiki wajitokeze kuona vifaa vipya walivyosajili kuelekea msimu mpya wa ligi kuuu Tanzania bara na michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Wachezaji-wa-timu-Yanga-wakifurahia-goli-la-pili-lililofungwa-na-Jerry-Tegete-kipindi-cha-pili-mnamo-dakika-ya-54-kwa-njia-ya-penati.-600x400Awali TFF walikataa timu hiyo kucheza mechi za kirafiki nchini kwa vile haikuwa na barua kutoka NFF, lakini sasa Shirikisho hilo limetoa idhini hiyo.
Pia ziara yake haikuwa inaratibiwa na wakala wa mechi anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) au mwanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Klabu hiyo kutoka Jimbo la Lagos ilipanga ziara hiyo kwa kuwasiliana na chama cha mpira wa miguu cha jimbo hilo ambacho nacho kilitakiwa kuomba idhini NFF kwa niaba ya 3Pillars.
Hivyo timu hiyo inaweza kucheza mechi, kwani ziara hiyo sasa inaratibiwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) ambaye ni mwanachama wetu.
TFF walikumbusha kuwa watu pekee wanaotakiwa kuandaa mechi za kirafiki za kimataifa ni mawakala wa mechi wanaotambuliwa na FIFA au wanachama wa TFF.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video