Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha wa Arsenal, Mzee, Arsene Wenger amethibitisha kuwa klabu yake inajitahidi kwa nguvu zote kusajili wachezaji wapya, lakini amekisifu kikosi chake cha sasa kuwa kina uwezo wa kupambana katika kinyang`anyiro cha ubingwa msimu ujao.
Wenger mpaka sasa amefanikiwa kusajili mchezaji mmoja wa bure, kinda wa miaka chini ya ishirini, Yaya Sanogo, kutoka nchini Ufaransa.
Klabu hiyo kwa sasa inataka kuvunja rekodi ya usajili na inaendelea kumuwinda mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez licha ya ofa yao ya pauni milioni 41 kutupiliwa mbali wiki iliyopita.
Namtaka yule pale: Kocha wa Arsenal , Arsene Wenger amethibitisha kuhitaji wachezaji wapya
Wenger amesema ” Bado tunafanya jitihada za kuimarisha kikosi kwa kusajili wachezaji wapya, lakini tunao wachezaji vijana walioanza kucheza ligi kuu kama Wojciech Szczesny, Carl Jenkinson, Alex Oxlade-Chamberlain”.
Kocha huyo anayesemekana kuwa mchumi zaidi alisema anaamini kikosi chake ni kizuri na kitaendelea kuwa kizuri zaidi, kwani vijana wake wanaweza kufanya mazuri zaidi, hivyo anajiamini kuwa msimu ujao watapambana vibaya sana kuhitaji taji.
Atajiunga? Luis Suarez amekuwa akihusishwa na kujiunga na Asernal, lakini Liverpool wanazingua
Wenger alikuwa anaongea Google Hangout ambapo mashabiki walikuwa wanamuuliza maswali moja kwa moja
0 comments:
Post a Comment