Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akielezea kufurahiswa kwake na ukuaji wa mchezo wa ngumi hapa nchini alipokutana na Bondia maarufu duniani na aliyewahi kuwa bingwa wa dunia mara mbili Francois Botha (White Buffalo) kushoto jana jijini Dar es Salaa.Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akiwa na Bingwa wa duni mara mbili wa mchezo wa ngumi Bondia Francois Botha (White Buffalo) wakipiga picha baada ya kukabidhiwa zawadi ya picha ya bondia huyo ikionyesha enzi za ujana wake jana jijini Dar es Salaam. Botha yupo nchini kufuatia kuwepo kwa pambano la ngumi la dunia litakalofanyika kesho huku likiwakutanisha mabondia Francis Cheka wa Tanzania na Phill William wa Marekani.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt fenella Mukangara na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo waliokaa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara na wageni walioambatana na Botha jana jijini Dar es Salaam.Bingwa wa duni mara mbili wa mchezo wa ngumi Bondia Francois Botha (White Buffalo) akielezea jambo kwa waandishi wa habari alipotembelea ofisini kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara kulia jana jijini Dar es Salaam.Bingwa wa duni mara mbili wa mchezo wa ngumi Bondia Francois Botha (White Buffalo) akielezea jambo huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga akisikiliza kwa makini jana jijini Dar es Salaam. Botha yupo nchini kufuatia kuwepo kwa pambano la ngumi la dunia litakalofanyika kesho huku likiwakutanisha mabondia Francis Cheka wa Tanzania na Phill William wa Marekani.
0 comments:
Post a Comment