Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe akifungua mkutano wa wadau wa maandalizi ya Mpango Kabambe wa Maendeleo ya Mji wa Mpanda wa miaka 20 ijayo mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Maria Mjini Mpanda jana.
Na Kibada Kibada -Kibada
Watumishi wa Idara ya Ujenzi katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda Mkoa wa Katavi wamelaumiwa kwa kushindwa kusimamia miradi ya ujenzi na wamekuwa ndio chanzo cha miradi kujengwa chini ya kiwango na kuchelewa kumalizika kwa wakati
Kauhi hiyo ya wakushutumu watumishi wa Idara ya Ujenzi ilitolewa hapo jana na Mwenyeki wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Enock Gwambasa kwenye mkutano wa Wadau wa maandalizi ya Mpango kabambe wa Halmashauri ya mji wa Mpanda wa kipindi cha miaka 20
Alisema licha ya watumishi hao kupewa maelekezo mbalimbali na vikao husika vinavyo kuwa vimewapatia maelekezo ya kusimia miradi ya ujenzi iliyopo katika Halmashauri hiyo bado kumekuwepo na matatizo ya miradi kujengwa chini ya kiwango na kuchelewa kumalizika kwa wakati
Gwambasa alieleza kuwa watumishi hao wameshindwa kusimamia midadi hata hiyo midogo iliyopo katika Halmashauri ya Mji huo inatia mashaka wa watumishi hao kusimamia miradi mikubwa ambayo inategemea kufanywa na Halmashauri hiyo hivi karibuni
Aliitaja miradi hiyo inayotegemewa kufanywa na Halmashauri hiyo kuwa ni ujenzi wa barabara za rami katika mitaa ya Mji wa Mpanda na ujenzi wa soko kubwa la kisasa
Alisema hivi karibuni kikao cha kamati ya fedha na mipango kilimwagiza Mkurugenzi waHalmashauri ya Mji wa Mpanda kumwita mkandarasi aliye tengeneza matuta ya kuzuia mwendo kasi wa magari na pikipiki kuvunja watuta yalioko katika maeneo ya Kotazi na Majengo na Buzogwe baada ya kubainika yamejengwa chini ya kiwango kutokana na kutosimamiwa ipasavyo na watumishi wa idara hiyo wakati ujenzi ulipo kuwa ukifanyika
Alisema na tayari wameisha towa maelekezo kwa mkurugenzi kuhakikisha watumishi walio shindwa kusimamia ujenzi huo wa matuta ya barabarani wanakatwa asilimi 20 ya mshahara wao mwezi mmoja na wapewe na risiti zao
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Seleman Lukanga alisema tayari ameisha yapokea maagizo hayo na tayari ameanza kuyafanyia kazi malalamiko ya watumishi wa Idara hiyo ya ujenzi
Mapema mwaka huu katika Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji huu katika kikao chake kilicho fanyika katika ukumbi wa Chuo kikuu huria cha Mkoa wa Katavi madiwani waliilalamikia idara hiyo kwa kushindwa kusimia midadi na kuifanya ishindwe kumalizika kwa wakati na miradi kujengwa chini ya kiwango
0 comments:
Post a Comment