Sunday, August 11, 2013

P1040881Na Baraka Mpenja 
Wakata miwa wa Mashamba ya Miwa ya Manungu Turiani Mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar leo hii wanatarajia kufuta makosa ya kufunga mabao 3-1 na Yanga katika mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya maafande wa Jeshi la Magereza, Tanzania Prisons “Wajelajela”.
Mechi hiyo iliyovuta hisia za mashabiki wa soka mjini Morogoro itapigwa katika dimba la Jamhuri Mkoani humo na kushuhudiwa na mashabiki wa Wana TamTAM wenye machungu ya kuburuzwa na “Kwalalumpa Malysia”, Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Dar Young Africans.
AKizungumzia mechi hiyo baada ya kutafutwa na MATUKIO DUNIANI, meneja wa Mtibwa Sugar, David Bugoya amesema mechi hiyo ni muhimu kwao kwani kocha mkuu Mecky Mexime ataitumia kufuta makosa ya kikosi chake kwenye mchezo uliopita dhidi ya wanajangwani.
“Huu ni wakati wa maandalizi, mwalimu anaangalia wapi kikosi kinakuwa na matatizo na kuyafanyia kazi, mechi ya Yanga kuna makosa yalitugharimu na ndio maana tumeona umuhimu wa kucheza mechi na Prisons, hivyo itakuwa mechi nzuri sana kwetu”. Alisema Bugoya.
Kwa upande wa Prisons, katibu mkuu wa klabu hiyo Sadick Jumbe amesema kikosi chao kipo salama na leo hii watawatumia wachezaji wote waliowasajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu.
“Mtibwa Sugar ni moja kati ya timu kubwa hapa nchini na ndio maana tumeamua kucheza mechi nao, baada ya mechi ya leo, tutacheza na Burkinafaso ya hapa Morogoro na kutafuta mechi nyingine yoyote hapa, baada ya hapo tutaingia Dar es salaam ambapo tutapimana na Ruvu Shooting”. Alisema Sadick.
Mtibwa Sugar wataanza mitanange ya ligi kuu kwa kukumbana na wana Lambalamba Azam fc agosti 24 mwaka huu katika dimba la Manungu Complex, wakati kwa upande wa Prisons wataanzia mabatini Mlandizi mkoani Pwani kuoneshana kazi na Ruvu Shooting.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video