Na Ali Issa –Maelezo Zanzibar.
Wakulima wa Bonde la Bubwisudi Wilaya ya Magharibi Unguja wame iomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuandaa utaratibu wa kununua Mpunga wa wakulima wa Bonde hilo ili wakulima waweza kufaidika na matunda ya kilimo hicho kwa kupata pesa zitakazo wasaidia katika mahitaji yao yakila siku.

Hayo yamesemwa huko Bumbisudi na Diwani wa wadi hiyo Masuod Abrahaman Masuod wakati wa uzinduzi wa Maazimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yalio fanyika katika wadi ya Bubwisudi Wilayani humo.
Wamesema kumekuwa na mpunga wakutosha katika baadhi ya majumba ya wakulima ambao walilima kwa kujituma katika msimu uliopita na hatimae kufanikiwa kupata mavuno mazuri, hivyo baadhi ya wananchi wanahitaji kuuza mpunga kupata pesa ili ziwasaidie katika maisha yao lakini hawajui nani wa muuzie bidhaa hiyo.
Wamesema bidha wanayo ya kutosha hivyo,iwapo Serikali itaweza kuandaa mpango huoitawasaidia wakulima hao kuweza kupata pesa za matumizi na kujikwamuwa katika mahitaji yao.
“Natoa wito kwa seriakali waweke utaratibu wa kununua mpunga kwa wananchi, kwani huu mpunga upo kwa baadhi ya wakulima wanataka kuuza lakini hawamjuwi nani wamuuzie”,alisema Diwani huyo.
Aidha diwani huyo alisema kua hali ya uchumi katika shehia hiyo ni nzuri kwani wananchi wa Bubwisudi wote ni wakulima na wanajituma
ipasavyo kwa vile kilimo ni ajira wanayo itegemea.
ipasavyo kwa vile kilimo ni ajira wanayo itegemea.
Akielezea changamoto zinazo wakabili wakulima hao walisema kua kumekuwa na ada kubwa ya malipo ya umeme katika mashamba ya mpunga ya umwagiliaji maji haliambayo hushindwa kulipa umeme huo ipasavyo.
“Tunalipa elfu 30 kwa mwezi ploti moja ya mpunga wa umwagiliaji hiki ni kiwango kikubwa, tunaomba tusaidiwe ili kukidha mahitaji yetu”,
alisema Bi Fatuma Daud Katibu wa Sheha Shehia ya Bubwisudi.
alisema Bi Fatuma Daud Katibu wa Sheha Shehia ya Bubwisudi.
Wakulima hao walimueleza Diwani kua, wana kabiliwa na tatizo la wizi wa mazao, na wana nchi wahapo hadi sasa bado hawajaweza kuazisha
Polisi jamii suala ambalo lingeweza kusaidia kupambana na vitendo vibaya vya wizi na uhalifu.
Polisi jamii suala ambalo lingeweza kusaidia kupambana na vitendo vibaya vya wizi na uhalifu.
Mapena diwani katika shamra shamra hizo alifungua kituo cha Taarifa na maarifa za Ukatili wa Kijisia na unyanyasaji ili kukuza usawa wajinsia kwa watoto na kinamama, jambo linaloonekana kuenea kila pembe ya Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment