Wawakilishi wa timu mbalimbali zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo na mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom tayari kwa ajili ya kuanza kwa msimu wa ligi kuu 2013/2014. Pamoja nao katika picha ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo Kelvin Twisa,(Aliyeshikilia mpira) na Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba.
Dar es Salaam
Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Tanzania Bara Kampuni ya Vodacom leo imekabidhi vifaa kwa timu 14 shiriki za ligi hiyo vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh 400 Milioni.
Akizungumza kabla ya zoezi la kukabidhi vifaa hivyo kuanza, Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba pamoja na kuishukuru Vodacom kwa kutekeleza majukumu yake ya kimkataba amevitaka vilabu vya ligi kuu kuu ya Vodacom kuheshimu chapa ya mdhamini wakati wote wa mechu za ligi.
“Ninatoa wito kwa vilabu vyote kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini kama kanuni zinavyo sema, pia ninawaomba viongozi wote tuwe na Ushirikiano katika kuhakikisha ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa,”
Kama mzazi tusingependa kutumia kanuni na sharia kuadhibu klabu inayokwenda kinyume tunapenda kuona kila mmoja akimtendea haki mdhamini kama ambavyo nay eye anavyotimiza haki yake ya kutupatia vifaa hivi.”Aliongeza Saad
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa alisema kuwa vifaa hivyo viko tayari na anaamini timu zote zimejiandaa vya kutosha na tayari kuingia katika mtanange wa ligi.
“Tunajisikia furaha sana kufikia hapa leo na kukabidhi vifaa hivi tukitekeleza matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zineshajiandaa vizuri na sasa tupo tayari kuanza msimu mpya wa 2013/2014.’Alisema Twissa
Twissa aliongeza kuwa vifaa vipya vilivyo kabidhiwa ni pamoja na seti za jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, soksi, vilinda ugoko (shin guards), nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vifaa vingine.
Aidha, Pamoja na kukabidhi vifaa hivyo wao kama wadhamini wa ligi kuu pia wamefarijika kuona timu zote zimefanya maandalizi ya kutosha.
“Hii ni ishara tosha kuwa siku hadi siku ligi yetu imeendelea kuimarika na kuwa na ushindani mkubwa zaidi hakika tunajivunia kuwa sehemu ya mafanikio ya soka nchini,” alisema.
Twissa alihitimisha kwa kutoa wito kwa wadau wengine wenye malengo ya kukuza soka la Tanzania kujitokeza na kuongeza udhamini katika ligi ili kuleta tija zaidi huku akiendelea kuwakumbusha wanahabari wajibu wao wa kuitangaza ligi hususan vipaji
Hatudhamini kwa sababu ya viongozi wala jambo jengine lolote, Vodacom inadhamini ligi kwa sababu soka ni mchezo unaopendwa na ndio wenye washabiki wengi na hatimae kukuza vipaji.”Alisema Twissa na kuongeza. “Vyombo vya habari mnanafasi kubwa sana ya kutangaza vipaji na ligi yetu na sio kuandika habari hasi ambazo hazijengi tungepeda kuona wachezaji wetu wanakuwa maarufu kama wanavyojulikana kina Ronaldo, Rooney na wengine wa nje.”
|
0 comments:
Post a Comment